Home






MAAZIMIO YA KAZI
Kiswahili
DARASA LA SITA
MWAKA WA 2026
MUHULA WA III

School


To enable/disable signing area for H.O.D & Principal, click here to update signature status on your profile.




To enable/disable showing Teachers name and TSC Number, click here to update teacher details status on your profile.












Did you know that you can edit this scheme? Just click on the part you want to edit!!! (Shift+Enter creates a new line)


WK KIPINDI MADA KUU MADA NDOGO SHABAHA SHUGHULI ZA UFUNZAJI MASWALI DADISI NYENZO TATHMINI MAONI
1

KUFUNGUA SHULE

2

MTIHANI WA KUFUNGUA SHULE

8

MTIHANI WA KAZOLE

9

LIKIZO YA KAZOLE

10 3
Kusikiliza na Kuzungumza
Mazungumzo ya Kimuktadha - Miktadha rasmi
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

-kutambua miktadha rasmi katika mawasiliano ili kuitofautisha
-kutumia lugha katika miktadha rasmi ili kufanikisha mawasiliano
-Kuchangamkia matumizi ya lugha katika miktadha rasmi kuimarisha maadili yafaayo.
Mwanafunzi aelekezwe:
-kutambua miktadha mbalimbali kunakotumiwa lugha rasmi (k.v. ofisini, hospitalini)
-kusikiliza mazungumzo rasmi kwa kutazama maigizo kwenye vyombo vya kidijitali (k.v. video, rununu, runinga, tarakilishi)
-kushiriki katika maigizo ya mazungumzo ya miktadha rasmi akishirikiana na wenzake
-kushiriki katika mazungumzo rasmi nje ya darasa k.m. akiwa kwenye gwaride, majilisini n.k.
-kutambua nidhamu ya lugha inayozingatiwa katika mazingira rasmi (k.m lugha ya heshima na adabu anapowasiliana).
1. Ni wapi katika shughuli zetu za kila siku tunaitumia lugha rasmi? -2. Ni nini kinachofanya mazungumzo yawe rasmi?
Oxford Kiswahili Darasa la 6 uk. 126
-Vifaa vya kidijitali (video, rununu, tarakilishi)
-Picha
10 4
Kusikiliza na Kuzungumza
Kusoma
Kusoma
Mazungumzo ya Kimuktadha - Miktadha isiyo rasmi
Kusoma kwa Mapana
Kusoma kwa Mapana
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

-kutambua miktadha isiyo rasmi katika mawasiliano ili kuitofautisha
-kutumia lugha katika miktadha isiyo rasmi ili kufanikisha mawasiliano
-Kuchangamkia matumizi ya lugha katika miktadha isiyo rasmi kuimarisha maadili yafaayo.
Mwanafunzi aelekezwe:
-kutambua miktadha mbalimbali kunakotumiwa lugha isiyo rasmi (k.v. nyumbani, sokoni)
-kusikiliza mazungumzo yasiyo rasmi kwa kutazama maigizo kwenye vyombo vya kidijitali (k.v. video, rununu, runinga, tarakilishi)
-kushiriki katika maigizo ya mazungumzo ya miktadha yasiyo rasmi akishirikiana na wenzake
-kushiriki katika mazungumzo yasiyo rasmi kama vile uwanjani, kwenye bweni, katika safari ya kwenda nyumbani kutoka shuleni.
1. Ni wapi katika shughuli zetu za kila siku tunaitumia lugha isiyo rasmi? -2. Ni nini kinachofanya mazungumzo yawe yasiyo rasmi?
Oxford Kiswahili Darasa la 6 uk. 128
-Vifaa vya kidijitali (video, rununu, tarakilishi)
-Picha
Oxford Kiswahili Darasa la 6 uk. 131
-Vitabu mbalimbali
-Majarida na magazeti
-Vifaa vya kidijitali
11 1
Kusoma
Kuandika
Kuandika
Kusoma kwa Mapana
Insha za Maelezo
Insha za Maelezo
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

-kutambua aina mbalimbali za matini ili kuchagua inayomvutia
-kusoma matini aliyochagua ili kufaidika na ujumbe na lugha iliyotumiwa
-kufurahia usomaji wa aina mbalimbali za matini ili kupanua mawazo yake.
Mwanafunzi aelekezwe:
-kutambua matini zinazomvutia maktabani na mtandaoni
-kusoma matini alizochagua ili kufaidi ujumbe na lugha iliyotumiwa
-kutoa wenzake muhtasari wa kile alichosoma kwenye matini ili kupashana ujumbe na kuchocheana kusoma zaidi kwa ajili ya kujifurahisha
-kujadiliana na wenzake matini ambazo wamesoma kwa kuzingatia ukuzaji wa msamiati.
1. Ni habari zipi unazopenda kusoma kwenye matini? -2. Unazingatia nini unapochagua matini za kusoma?
Oxford Kiswahili Darasa la 6 uk. 131
-Vitabu mbalimbali
-Majarida na magazeti
-Vifaa vya kidijitali
Oxford Kiswahili Darasa la 6 uk. 135
-Vielelezo vya insha za maelezo
11 2
Sarufi
Kusikiliza na Kuzungumza
Kusikiliza na Kuzungumza
Vinyume vya Vivumishi
Sitiari za Tabia
Sitiari za Tabia
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

-kutambua vinyume vya vivumishi katika matini
-kutunga sentensi kwa kutumia vinyume vya vivumishi
-kuchangamkia matumizi ya vinyume vya vivumishi katika mawasiliano ya kila siku.
Mwanafunzi aelekezwe:
-kutambua vinyume vya vivumishi (k.v. zuri- baya, kali-butu, refu- fupi) katika chati, kadi za maneno, kapu la maneno, mti wa maneno au vifaa vya kidijitali
-kutafuta vinyume vya vivumishi kwa kurejelea orodha ya vivumishi alivyopewa
-kutalii mazingira yake na kuunda orodha ya vinyume vya vivumishi
-kutunga sentensi kwa kutumia vinyume vya vivumishi kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi.
Je, ni vivumishi vipi unavyoweza kutambua vinyume vyake?
Oxford Kiswahili Darasa la 6 uk. 137
-Chati
-Kadi za maneno
-Kapu la maneno
-Mti wa maneno
-Vifaa vya kidijitali
Oxford Kiswahili Darasa la 6 uk. 140
-Vitabu
-Matini mbalimbali
-Vyombo vya kidijitali
11 3
Kusoma
Kuandika
Kusoma kwa Mapana
Insha za Masimulizi
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

-kutambua na kufungua faili iliyo na kifungu cha kusoma ili kuimarisha umilisi wake wa kutumia tarakilishi
-kuonyesha uelewa wa hatua za kiusalama kwa kusakura matini kwenye tovuti salama ili kupata vifungu vya kusoma kutumia vyombo vya kidijitali
-kuchangamkia matumizi ya vifaa vya kidijitali katika kutafuta na kusoma ujumbe ili kuimarisha maarifa yake.
Mwanafunzi aelekezwe:
-kutambua mambo ya kuzingatia anaposoma matini zilizohifadhiwa katika kifaa cha kidijitali (k.v. kutofuta kazi za wenzake zilizohifadhiwa katika vifaa vya kidijitali) akishirikiana na wenzake
-kutambua mambo ya kuzingatia anaposoma matini za mtandaoni (k.v. kufungua mitandao ifaayo, kutowasiliana na watu usiowajua, kutofichua nywila yako kwa wenzake)
-kutambua jina la faili lengwa kwenye tarakilishi na kufanya mazoezi ya kufungua na kufunga
-kutambua mitandao salama yenye matini inayoafiki kiwango na mahitaji yake
-kutambua umuhimu wa kutoa habari kwa mwalimu, mzazi au mlezi wake endapo atapata ujumbe kutoka kwa watu asiowajua mtandaoni na kutowasiliana nao
-kutafuta maana za maneno mapya kwenye kamusi mtandaoni, kusimulia wenzake habari alizosoma.
1. Unakumbuka habari gani uliyoisoma mtandaoni? -2. Ni hatua gani za kiusalama unazozingatia unapotafuta habari mtandaoni?
Oxford Kiswahili Darasa la 6 uk. 142
-Vifaa vya kidijitali (tarakilishi)
-Kamusi ya mtandaoni
Oxford Kiswahili Darasa la 6 uk. 147
-Vielelezo vya insha
-Vifaa vya kidijitali
11 4
Kuandika
Sarufi
Sarufi
Insha za Masimulizi
Hali ya Masharti
Hali ya Masharti
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

-kueleza maudhui ya insha ya masimulizi ili kuandika ifaavyo
-kuandika insha ya masimulizi kwa kufuata kanuni zifaazo
-kuchangamkia utunzi mzuri ili kuimarisha mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwe:
-kutambua insha ya masimulizi kwa kurejelea vielelezo vya insha zilizoandikwa kwenye matini mbalimbali au tarakilishi
-kujadili mada na vidokezo vya insha ili kuvitumia katika kuandika insha yake
-kuelezea maudhui atakayotumia kuandikia insha ya masimulizi
-kuandika insha ya masimulizi (k.v. kuhusu ugaidi, uhalifu, ajali, safari n.k) isiyopungua maneno 200 akizingatia mada, mpangilio mzuri wa mawazo, hati safi, tahajia, kanuni za kisarufi, uakifishaji mwafaka, lugha ya kiubunifu na urefu unaotarajiwa. Pia azingatie aina mbalimbali za maneno, mnyambuliko wa vitenzi, na nyakati ili kejenga picha dhahiri ya anachokiandikia daftarini
-kuandika insha ya masimulizi katika vifaa vya kidijitali na kuisambaza kwa wenzake na mwalimu ili kuisoma na kuitathmini
-kuwawasilishia wenzake insha aliyoandika ili waitathmini na kumwelekeza.
Insha ya masimulizi ina sifa gani?
Oxford Kiswahili Darasa la 6 uk. 147
-Vielelezo vya insha
-Vifaa vya kidijitali
Oxford Kiswahili Darasa la 6 uk. 151
-Chati
-Ubao
12 1
Sarufi
Kusikiliza na Kuzungumza
Kusikiliza na Kuzungumza
Hali ya Masharti
Kuzungumza na Kujieleza kwa Ufasaha
Kuzungumza na Kujieleza kwa Ufasaha
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

-kutambua viambishi vya hali ya masharti kwenye kitenzi
-kutumia vitenzi katika hali ya masharti kwenye sentensi
-kufurahia matumizi ya hali ya masharti katika mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwe:
-kutambua viambishi vya hali ya masharti (nge, ngali, ki) kwenye vitenzi katika chati, ubao au kwa kutumia vifaa vya kidijitali
-kutumia vitenzi vya hali ya masharti katika sentensi kwa kuandika daftarini au kupiga chapa kwenye tarakilishi/kipakatalishi
-kubadilisha sentensi kutoka hali moja hadi nyingine
-kutunga sentensi katika hali ya mazoea na hali ya masharti mtandaoni na kuwatumia wenzake waweze kuzisoma na kutathmini usahihi wake.
Je, unajua viambishi vipi?
Oxford Kiswahili Darasa la 6 uk. 151
-Chati
-Ubao
-Vifaa vya kidijitali
Oxford Kiswahili Darasa la 6 uk. 155
-Tepurekoda
-Video
-Tarakilishi
-Mgeni mwalikwa
Oxford Kiswahili Darasa la 6 uk. 156
12 2
Kusoma
Kuandika
Kusoma kwa Ufasaha
Barua Rasmi
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

-kutambua vipengele vya kuzingatia katika kusoma kwa ufasaha
-kusoma kifungu kwa kuzingatia matamshi bora
-kusoma kifungu kwa kasi ifaayo
-kusoma kifungu kwa kutumia sauti ipasavyo
-kusoma kifungu kwa kuambatanisha ishara zifaazo
-kuchangamkia kusoma kifungu kwa kuzingatia vipengele vya usomaji.
Mwanafunzi aelekezwe:
-kujadiliana na wenzake vipengele vya kuzingatia katika kusoma makala kwa ufasaha
-kusoma kifungu kuhusu suala lengwa katika matini andishi au ya kidijitali akizingatia matamshi bora
-kusoma kifungu cha habari kwa kasi ifaayo kuhusu suala lengwa
-kusoma kifungu akizingatia sauti ifaayo (k.v. kiwango cha sauti na kiimbo)
-kusoma kifungu kwa kuambatanisha ishara zifaazo panapofaa (k.v. ishara za uso na mikono zinazozingatia tamaduni)
-kushirikiana na mzazi au mlezi kusoma makala akizingatia vipengele vya usomaji bora.
Je, kusoma kwa ufasaha kuna umuhimu gani?
Oxford Kiswahili Darasa la 6 uk. 157
-Maandishi mbalimbali
-Vifaa vya kidijitali
Oxford Kiswahili Darasa la 6 uk. 160
-Kielelezo cha barua rasmi
-Tarakilishi
12 3
Kuandika
Sarufi
Sarufi
Sarufi
Barua Rasmi
Ukanushaji wa Maneno
Ukanushaji wa Maneno
Ukanushaji wa Maneno
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

-kujadili maudhui ili kuandika barua rasmi inayozingatia mada
-kuandika barua rasmi inayozingatia mada, hati safi, muundo na mtindo ufaaoili kuwasiliana ipasavyo
-kuchangamkia utunzi wa barua rasmi katika mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwe:
-kutambua mada ya kuandikia barua rasmi
-kujadili na wenzake maudhui yafaayo kulingana na mada ya insha ya barua rasmi
-kuandika vidokezo vya kumwongoza
-kujadili na wenzake vipengele vya aya
-kuandika barua rasmi kwa mwalimu daftarini kuomba msamaha na kuiwasilisha kila hoja katika aya yake
-kutumia sentensi inayobeba wazo kuu mwanzoni mwa kila aya
-kuandika kwa hati safi au kwa kutumia tarakilishi huku akizingatia kanuni zifaazo
-kujadiliana na wenzake kuhusu umuhimu wa barua rasmi katika mawasiliano.
1. Uandishi wa barua rasmi huzingatia vipengele gani? -2. Unazingatia nini ili kuunda aya nzuri?
Oxford Kiswahili Darasa la 6 uk. 160
-Kielelezo cha barua rasmi
-Tarakilishi
Oxford Kiswahili Darasa la 6 uk. 162
-Vitabu
-Vifaa vya kidijitali
12 4
Sarufi
Ukubwa na Udogo wa Nomino
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

-kutambua nomino zinazoanza kwa kiambishi Ki- katika kundi la maneno
-kubadilisha nomino, zinazoanza kwa Ki- katika hali wastani kuwa katika hali ya ukubwa na udogo
-kutunga sentensi sahihi akitumia nomino zinazoanza kwa Ki- katika hali ya ukubwa na udogo huku akizingatia upatanisho wa kisarufi
-kufurahia kutumia nomino zinazoanza kwa Ki- kwa usahihi katika hali ya ukubwa na udogo ili kuimarisha mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwe:
-kutambua nomino zinazoanza kwa kiambishi Ki- (k.v. kiti, kitabu, kitanda) kwa kutumia kadi za maneno, mti wa maneno, chati au vifaa vya kidijitali
-kushiriki kwenye mjadala wa kutambua viambishi vinavyotumika kudhihirisha ukubwa na udogo wa nomino
-kushiriki katika vikundi kubadilisha nomino kutoka hali ya wastani hadi hali ya ukubwa na udogo
-kushiriki katika mchezo wa vikundi ambapo kikundi kimoja kitataja wastani wa nomino na kingine kutaja ukubwa na udogo wa nomino hiyo
-kutunga sentensi kwa kutumia nomino hizo katika hali ya ukubwa na udogo kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi.
Je, ni nomino gani zinazoanza kwa kiambishi Ki- unazozijua?
Oxford Kiswahili Darasa la 6 uk. 164
-Kadi za maneno
-Mti wa maneno
-Chati
-Vifaa vya kidijitali
13 1
Sarufi
Ukubwa na Udogo wa Nomino
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

-kutambua nomino zinazoanza kwa kiambishi Ki- katika kundi la maneno
-kubadilisha nomino, zinazoanza kwa Ki- katika hali wastani kuwa katika hali ya ukubwa na udogo
-kutunga sentensi sahihi akitumia nomino zinazoanza kwa Ki- katika hali ya ukubwa na udogo huku akizingatia upatanisho wa kisarufi
-kufurahia kutumia nomino zinazoanza kwa Ki- kwa usahihi katika hali ya ukubwa na udogo ili kuimarisha mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwe:
-kutambua nomino zinazoanza kwa kiambishi Ki- (k.v. kiti, kitabu, kitanda) kwa kutumia kadi za maneno, mti wa maneno, chati au vifaa vya kidijitali
-kushiriki kwenye mjadala wa kutambua viambishi vinavyotumika kudhihirisha ukubwa na udogo wa nomino
-kushiriki katika vikundi kubadilisha nomino kutoka hali ya wastani hadi hali ya ukubwa na udogo
-kushiriki katika mchezo wa vikundi ambapo kikundi kimoja kitataja wastani wa nomino na kingine kutaja ukubwa na udogo wa nomino hiyo
-kutunga sentensi kwa kutumia nomino hizo katika hali ya ukubwa na udogo kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi.
Je, ni nomino gani zinazoanza kwa kiambishi Ki- unazozijua?
Oxford Kiswahili Darasa la 6 uk. 164
-Kadi za maneno
-Mti wa maneno
-Chati
-Vifaa vya kidijitali
Oxford Kiswahili Darasa la 6 uk. 167

Your Name Comes Here


Download

Feedback