Home






MAAZIMIO YA KAZI
Kiswahili
DARASA LA TANO
MWAKA WA 2025
MUHULA WA III

School


To enable/disable signing area for H.O.D & Principal, click here to update signature status on your profile.




To enable/disable showing Teachers name and TSC Number, click here to update teacher details status on your profile.












Did you know that you can edit this scheme? Just click on the part you want to edit!!! (Shift+Enter creates a new line)


WK KIPINDI MADA KUU MADA NDOGO SHABAHA SHUGHULI ZA UFUNZAJI MASWALI DADISI NYENZO TATHMINI MAONI
1 1
MAADILI

Kusikiliza na Kuzungumza
Kusoma
Ushairi
Kusoma kwa Mapana: Makala
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo,
- Kukariri shairi kwa kuzingatia matamshi na mahadhi mbalimbali
- Kueleza maana ya msamiati uliotumiwa katika shairi
- Kutumia msamiati uliotumiwa katika shairi kuboresha masiliano
- Kuonyesha ufahamu wa ujumbe katika shairi kwa kujibu maswali
- Kuchangamkia ushairi kama njia ya kujieleza kwa ufasaha
Mwanafunzi aelekezwe:
- Kukariri shairi kuhusu mada lengwa (maadili) kwa kuzingatia matamshi na mahadhi mbalimbali
- Kusikiliza shairi lengwa likikaririwa au kuimbwa na mwalimu, mgeni mwalikwa (mghani) au kupitia vifaa vya kidijitali
- Kushirikiana na wenzake kukariri au kuimba shairi kwa mahadhi mbalimbali
- Kutambua msamiati uliotumika katika ushairi kuhusu maadili (k.m. haki, usawa, heshima na uwajibikaji) na kuueleza akiwa peke yake au kwa kushirikiana na wenzake
Ushairi unaweza kuboresha mazungumzo yako vipi?
Mentor Kiswahili Gredi ya 5 uk. 94
Chati ya shairi la "Nawajibika"
Vifaa vya kidijitali
Kamusi
Mentor Kiswahili Gredi ya 5 uk. 96
Makala mbalimbali
Kukariri shairi kwa kuzingatia mahadhi Kueleza maana ya msamiati uliotumiwa katika shairi Kujibu maswali kuhusu ujumbe wa shairi Kutumia msamiati wa shairi kutunga sentensi
1 2
Sarufi
Ngeli ya U-YA
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo,
- Kutambua nomino katika ngeli ya U-YA ili kuzitofautisha na nomino katika ngeli nyingine
- Kuandika nomino za ngeli ya U-YA katika umoja na wingi
- Kuandika umoja na wingi wa mafungu ya maneno katika ngeli ya ngeli ya U-YA
- Kuchangamkia kutumia nomino za ngeli ya U-YA katika mawasiliano
Mwanafunzi aelekezwe:
- Kutambua nomino zinazoanza kwa herufi u- katika umoja na zinazoanza kwa ma- katika wingi
- Kutambua nomino katika ngeli ya U-YA kwenye chati, ubao, mti maneno, kapu la maneno au kifaa cha kidijitali
- Kupiga mstari viambishi vipatanishi vya ngeli ya U-YA katika sentensi
- Kujaza nafasi kwa viambishi vifaavyo vya ngeli ya U-YA
Je, nomino za ngeli ya U-YA huchukua viambishi gani katika sentensi?
Mentor Kiswahili Gredi ya 5 uk. 100
Kadi maneno
Chati ya nomino za ngeli ya U-YA
Picha zenye nomino za ngeli ya U-YA
Kutambua nomino za ngeli ya U-YA Kuandika nomino za ngeli ya U-YA katika umoja na wingi Kutambua viambishi vipatanishi vya ngeli ya U-YA Kujaza nafasi kwa viambishi sahihi vya ngeli ya U-YA
1 3
Kuandika
Kusikiliza na Kuzungumza
Insha ya Wasifu
Ushairi
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo,
- Kutambua vipengele vya kimuundo vya insha za wasifu
- Kuandika insha ya wasifu kwa kuzingatia muundo na mtindo ufaao
- Kufurahia uandishi wa insha za wasifu ili kukuza stadi ya kuandika
Mwanafunzi aelekezwe:
- Kutambua insha ya wasifu kwa kurejelea vielelezo vya insha zilizoandikwa kwenye matini mbalimbali au tarakilishi
- Jadilini sehemu mbalimbali za insha ya wasifu vifuatavyo kwenye insha mliyosoma: kichwa, utangulizi, mwili na hitimisho
- Jikiteni jinsi mada yenyewe, utangulizi, mwili na hitimisho vinaweza kumwelezea mtu, kitu, mnyama au mahali
Unazingatia nini unapoandika insha ya wasifu?
Mentor Kiswahili Gredi ya 5 uk. 98
Insha za wasifu
Vifaa vya kidijitali
Mchoro wa muundo wa insha ya wasifu
Mentor Kiswahili Gredi ya 5 uk. 95
Mashairi mbalimbali
Uchati wa msamiati wa maadili
Kutambua vipengele vya muundo vya insha ya wasifu Kuchora mchoro wa muundo wa insha ya wasifu Kueleza vipengele vinavyojenga insha ya wasifu Kutofautisha insha ya wasifu na aina nyingine za insha
1 4
Kusoma
Sarufi
Kusoma kwa Mapana: Makala
Ngeli ya U-YA
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo,
- Kutambua makala ya kusoma katika maktaba ili kuimarisha uchaguzi bora wa makala
- Kusoma makala mbalimbali ili kujenga ufasaha wa lugha
- Kufurahia kusoma makala mbalimbali ili kujenga ufasaha wa lugha
Mwanafunzi aelekezwe:
- Tambua maneno usiyojua maana zake katika makala mliyosoma
- Tumia kamusi kueleza maana za msamiati huo
- Wasilisha kazi yako kwa mwalimu na wenzako
- Waombe wakutolee maoni
Unapenda kusoma makala ya aina gani?
Mentor Kiswahili Gredi ya 5 uk. 97
Kamusi
Makala mbalimbali
Vifaa vya kidijitali
Mentor Kiswahili Gredi ya 5 uk. 101
Chati ya viambishi vya ngeli ya U-YA
Kadi maneno
Kutambua msamiati katika makala Kueleza maana ya msamiati kwa kutumia kamusi Kutoa maoni kuhusu ujumbe wa makala Kutumia msamiati katika sentensi
2 1
Kuandika
Kusikiliza na Kuzungumza
Insha ya Wasifu
Nahau: Nahau za Usafi na Mazingira
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
Mwisho wa funzo,
- Kutambua vipengele vya kimuundo vya insha za wasifu
- Kuandika insha ya wasifu kwa kuzingatia muundo na mtindo ufaao
- Kufurahia uandishi wa insha za wasifu ili kukuza stadi ya kuandika
Mwanafunzi aelekezwe:
- Chagua mada ya kutungia insha ya wasifu
- Jadili kuhusu mada uliyochagua na wenzako darasani
- Andaa vidokezo ambavyo vitakuongoza kuandika insha ya wasifu kuhusu mada uliyochagua
- Andika insha ya wasifu kwa kuzingatia vidokezo ulivyoandaa
Je, ni mada gani zinafaa kuandikiwa insha ya wasifu?
Mentor Kiswahili Gredi ya 5 uk. 99
Vifaa vya kidijitali
Orodha ya vipengele vya insha ya wasifu
Miongozo ya kuandika insha ya wasifu
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 104
Picha za nahau mbalimbali
Kadi za maneno
Chati ya nahau
Kuandika insha ya wasifu kwa kuzingatia muundo ufaao Kutumia lugha ya kiubunifu kuandika insha Kusahihisha makosa katika insha Kutoa tathmini ya insha za wenzake
2 2
ELIMU YA MAZINGIRA

Kusoma
Kusoma
Sarufi
Kusoma kwa Mapana: Matini
Ngeli ya KU-KU
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- kutambua matini anazotaka kusoma kwenye maktaba
- kusoma matini ili kufaidika na ujumbe na lugha inayotumiwa
- kufurahia usomaji wa matini za aina mbalimbali ili kujenga utamaduni wa kusoma
Mwanafunzi aelekezwe:
- kutambua aina mbalimbali za matini (kama vile vitabu, magazeti, na majarida) kwenye maktaba, tarakilishi au kadi za katalogi
- kutazama picha za matini mbalimbali na kujadili kuhusu aina za matini
- kujadili kuhusu nini kinachoonekana kwenye picha za matini mbalimbali
- kutambua matini ya kujisomea maktabani au mtandaoni
- kutambua matini inayomvutia kuisoma
1. Unapenda kusoma matini ya aina gani? 2. Ni vipi unavyoweza kupata matini ya kusoma? 3. Kusoma aina mbalimbali za matini kuna umuhimu gani?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 107
Picha za matini mbalimbali
Vitabu, magazeti na majarida
Vifaa vya kidijitali
Matini mbalimbali
Maktaba
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 112
Picha za vitendo
Sentensi zilizo na nomino za ngeli ya KU-KU
Orodha ya nomino za ngeli ya KU-KU
Kutambua aina mbalimbali za matini Kusoma matini aliyochagua Kueleza aina za matini Kujibu maswali kuhusu matini
2 3
Sarufi
Kuandika
Kusikiliza na Kuzungumza
Ngeli ya KU-KU
Kuandika Insha: Insha ya Maelezo
Nahau: Nahau za Usafi na Mazingira
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- kutambua nomino katika ngeli ya KU-KU
- kuandika nomino za ngeli ya KU-KU katika umoja na wingi
- kuandika umoja na wingi wa mafungu ya maneno katika ngeli ya KU-KU
- kuchangamkia kutumia nomino za ngeli ya KU-KU katika mawasiliano
Mwanafunzi aelekezwe:
- kutazama picha zinazoonyesha vitendo mbalimbali na kutaja vitendo hivyo
- kutaja nomino za ngeli ya KU-KU kutokana na vitendo katika picha
- kutaja nomino nyingine za ngeli ya KU-KU
- kuchagua nomino za ngeli ya KU-KU kwenye mti maneno
- kuunda nomino za ngeli ya KU-KU kwa kutumia kiambishi ku- na kitenzi
- kuandika sentensi katika umoja na wingi
- kutunga sentensi kwa kutumia nomino za ngeli ya KU-KU
1. Ni vipi tunaweza kuunda nomino za ngeli ya KU-KU? 2. Je, nomino za ngeli ya KU-KU zinatofautiana vipi na nomino za ngeli nyingine?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 113
Picha za vitendo
Mti maneno
Jedwali la kuundika nomino za ngeli ya KU-KU
Vifaa vya kidijitali
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 109
Matini ya insha ya maelezo
Mifano ya insha za maelezo
Chati ya muundo wa insha
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 105
Orodha ya nahau
Picha zinazoonyesha nahau mbalimbali
Kuunda nomino za ngeli ya KU-KU Kutambua nomino za ngeli ya KU-KU Kuandika sentensi katika umoja na wingi Kutunga sentensi zenye nomino za ngeli ya KU-KU
2 4
Kusoma
Sarufi
Kusoma kwa Mapana: Matini
Ngeli ya KU-KU
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- kutambua matini anazotaka kusoma kwenye maktaba
- kusoma matini ili kufaidika na ujumbe na lugha inayotumiwa
- kufurahia usomaji wa matini za aina mbalimbali ili kujenga utamaduni wa kusoma
Mwanafunzi aelekezwe:
- kusoma matini aliyoichagua ili kupata ujumbe uliomo
- kueleza ujumbe wa matini hiyo kwa ufupi
- kuandika muhtasari wa matini aliyoisoma
- kuwasilisha muhtasari wake kwa wenzake ili wausikilize na kuutolea maoni
- kutoa maoni yake kuhusu matini aliyoisoma
- kujadiliana na wenzake kuhusu matini mbalimbali walizozisoma
1. Ulipata ujumbe gani kutoka kwa matini uliyosoma? 2. Unaweza kushauri wenzako wasome matini hiyo? Kwa nini?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 108
Matini mbalimbali
Daftari za wanafunzi
Vifaa vya kidijitali
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 115
Sentensi zenye viambishi vya ngeli ya KU-KU
Tepurekoda au kinasasauti
Kueleza ujumbe wa matini aliyosoma Kuandika muhtasari wa matini Kuwasilisha muhtasari Kutoa maoni kuhusu matini
3 1
Sarufi
Kuandika
Ngeli ya KU-KU
Kuandika Insha: Insha ya Maelezo
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- kutambua viambishi vipatanishi vya ngeli ya KU-KU kwenye sentensi
- kuunda sentensi akitumia nomino za ngeli ya KU-KU katika umoja na wingi akizingatia upatanisho wa kisarufi
- kufurahia matumizi ya ngeli ya KU-KU katika mawasiliano
Mwanafunzi aelekezwe:
- kusikiliza sentensi zikisomwa katika kiungo kilichotolewa
- kutambua nomino za ngeli ya KU-KU kwenye sentensi alizosikiliza
- kutumia kiambishi cha ngeli ya KU-KU kujaza kila nafasi kwa usahihi
- kuandika nomino tano za ngeli ya KU-KU
- kuchagua nomino ya ngeli ya KU-KU kwenye orodha iliyotolewa kujazia kila pengo
- kutunga sentensi zenye nomino za ngeli ya KU-KU
1. Je, kuna nomino gani nyingine za ngeli ya KU-KU ambazo hujazitaja bado? 2. Je, ni viambishi gani vya ngeli ya KU-KU hutumika katika umoja na wingi?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 116
Kiungo cha sauti:
Orodha ya nomino za ngeli ya KU-KU
Sentensi zenye nafasi za kujaza
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 111
Daftari la mwanafunzi
Mifano ya insha za maelezo
Vidokezo vya kuandaa insha
Kujaza nafasi kwa viambishi vya ngeli ya KU-KU Kutambua nomino za ngeli ya KU-KU Kutunga sentensi zenye nomino za ngeli ya KU-KU Kufafanua matumizi ya viambishi vya ngeli ya KU-KU
3 2
NDEGE WA PORINI

Kusikiliza na Kuzungumza
Kusoma
Visawe
Kusoma kwa Ufahamu: Mchezo wa Kuigiza
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- kutambua maneno matatu yenye maana sawa katika matini
- kutumia visawe ifaavyo katika mawasiliano
- kuthamini matumizi ya visawe katika mawasiliano
Mwanafunzi aelekezwe:
- kutambua maneno matatu yenye maana sawa (k.v. nyumbani, mastakimu, chengo; barabara, tariki, baraste; jitimai, huzuni, simanzi) kwa kutumia kapu la maneno, kadi za maneno, mti maneno au kuburura kwa kutumia tarakilishi
- kueleza maana ya maneno matatu yenye maana sawa akiwa na wenzake
- kuambatanisha maneno matatu yenye maana sawa kutoka kapu maneno, mti maneno, ubao, chati, vyombo vya kidijitali, kadi maneno
- kuhusisha visawe na vifaa halisi, picha, michoro kwenye chati, kitabu au vyombo vya kidijitali
- kujadili visawe mbalimbali katika vikundi
Unajua maneno gani yenye maana sawa?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 118
Picha za ndege wa porini
Kadi za maneno
Kapu la maneno
Mti maneno
Vifaa vya kidijitali
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 121
Mchezo wa kuigiza "SHIDA TUNAZOKABILIANA NAZO"
Orodha ya wahusika
Kutambua maneno matatu yenye maana sawa Kueleza maana ya visawe Kuambatanisha maneno matatu yenye maana sawa Kutunga sentensi kwa kutumia visawe
3 3
Kusoma
Kusoma kwa Ufahamu: Mchezo wa Kuigiza
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- kutambua mchezo wa kuigiza katika matini
- kusoma mchezo mfupi wa kuigiza kwa ufasaha
- kueleza maana ya msamiati uliotumiwa katika mchezo wa kuigiza
- kuonyesha ufahamu wa mchezo wa kuigiza kwa kujibu maswali
- kuigiza mchezo mfupi ili kukuza uwezo wa kujieleza
- kufurahia kusoma michezo na kuigiza
Mwanafunzi aelekezwe:
- kueleza maana za maneno kama vile 'mwewe', 'mbuni', 'chiriku', 'kasuku' na 'kukuziwa' jinsi yalivyotumika katika mchezo wa kuigiza
- kuandika ujumbe wa mchezo wa kuigiza kwa ufupi
- kuwasilisha muhtasari wa mchezo wa kuigiza kwa wenzake ili wautolee maoni
- kuigiza mchezo wa kuigiza kwa kuhakikisha wametilia mkazo maelekezo yaliyotolewa
- kusoma video ya mchezo wa kuigiza katika mtandao salama
- kujadili maelekezo yaliyotumiwa kwenye mchezo huo
1. Je, ujumbe wa mchezo wa kuigiza "SHIDA TUNAZOKABILIANA NAZO" ni upi? 2. Ni matatizo gani yanayowakumba ndege wa porini?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 123
Mchezo wa kuigiza ulioandikwa
Video za mchezo wa kuigiza
Kamusi ya Kiswahili
Kueleza maana ya maneno Kuandika muhtasari wa mchezo wa kuigiza Kuigiza mchezo wa kuigiza kwa kuzingatia maelekezo Kujadili ujumbe wa mchezo wa kuigiza
3 4
Sarufi
Mnyambuliko wa Vitenzi: Kauli ya Kutendewa
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- kutambua vitenzi katika hali ya kutendewa katika matini ili kuvitofautisha
- kutumia vitenzi katika hali ya kutendewa ipasavyo anapowasiliana
- kuchangamkia matumizi ya vitenzi katika hali ya kutendewa katika mawasiliano ya kila siku
Mwanafunzi aelekezwe:
- kutazama picha zinazoonyesha vitendo vinavyofanyiwa watu (k.v. somewa, pewa, bebewa, ombewa)
- kujadili vitendo vinavyofanyiwa wahusika katika picha
- kueleza kuwa vitenzi somewa, pewa, bebewa na ombewa viko katika kauli ya kutendewa
- kutambua vitenzi katika kauli ya kutendewa kwenye orodha ya vitenzi (chorewa, limia, pikiwa, imbia, andikiwa)
- kupigia mstari vitenzi katika kauli ya kutendewa kwenye sentensi
- kuchagua sentensi zilizotumia vitenzi katika kauli ya kutendewa
Je, vitenzi vinabadilika vipi vikiongezewa viambishi?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 128
Picha zinazoonyesha watu wakifanyiwa vitendo
Orodha ya vitenzi
Sentensi zenye vitenzi katika kauli ya kutendewa
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 129
Jedwali la vitenzi katika kauli ya kutenda na kutendewa
Daftari la mwanafunzi
Kutambua vitenzi katika hali ya kutendewa Kupigia mstari vitenzi katika kauli ya kutendewa Kuchagua sentensi zenye vitenzi katika kauli ya kutendewa Kueleza maana ya kauli ya kutendewa
4 1
Sarufi
Mnyambuliko wa Vitenzi: Kauli ya Kutendeka
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- kutambua vitenzi katika hali ya kutendeka katika matini ili kuvitofautisha
- kutumia vitenzi katika hali ya kutendeka ipasavyo anapowasiliana
- kuchangamkia matumizi ya vitenzi katika hali ya kutendeka katika mawasiliano ya kila siku
Mwanafunzi aelekezwe:
- kutazama picha zinazoonyesha vitendo (futika, funguka, shoneka, limika)
- kujadili kinachofanyika kwenye picha hizo
- kusoma vitenzi kwenye picha hizo
- kueleza kwamba vitenzi hivyo viko katika kauli ya kutendeka
- kutaja vitenzi vitano vingine katika kauli ya kutendeka
- kuchagua vitenzi katika kauli ya kutendeka kwenye chati
- kupigia mstari vitenzi katika kauli ya kutendeka kwenye sentensi
- kuchagua sentensi zilizo na vitenzi katika kauli ya kutendeka
Je, ni vitenzi vipi viko kwenye kauli ya kutendeka?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 130
Picha zinazoonyesha vitendo katika kauli ya kutendeka
Chati ya vitenzi
Sentensi zenye vitenzi vya kauli ya kutendeka
Kutambua vitenzi katika kauli ya kutendeka Kutaja vitenzi katika kauli ya kutendeka Kupigia mstari vitenzi katika kauli ya kutendeka Kuchagua sentensi zenye vitenzi katika kauli ya kutendeka
4 2
Kuandika
Kusikiliza na Kuzungumza
Insha za Masimulizi
Visawe
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- kueleza sifa za insha ya masimulizi ili kuibainisha
- kuandika insha ya masimulizi kwa kufuata kanuni zifaazo
- kuchangamkia utunzi mzuri
Mwanafunzi aelekezwe:
- kusoma insha ya masimulizi kuhusu "CHANZO CHA TABIA ZA NDEGE"
- kutambua sifa za insha ya masimulizi
- kupambanua sehemu za insha hiyo (mada, utangulizi, mwili, hitimisho)
- kujadili maudhui ya insha hiyo
- kuandika vidokezo vya insha tofauti ya masimulizi kuhusu ndege wa porini
- kujadiliana na wenzake kuhusu vidokezo hivyo
Ni mambo gani unayozingatia ili kuandika insha ya masimulizi ya kuvutia?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 126
Insha ya masimulizi "CHANZO CHA TABIA ZA NDEGE"
Chati ya sifa za insha ya masimulizi
Daftari la mwanafunzi
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 119
Kadi za visawe
Jedwali la kuambatanisha maneno na visawe
Sentensi zenye maneno yaliyopigiwa mstari
Kutambua sifa za insha ya masimulizi Kupambanua sehemu za insha ya masimulizi (mada, utangulizi, mwili, hitimisho) Kueleza maudhui ya insha ya masimulizi Kuandika vidokezo vya insha ya masimulizi
4 3
Kusoma
Kusoma kwa Ufahamu: Mchezo wa Kuigiza
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- kutambua mchezo wa kuigiza katika matini
- kusoma mchezo mfupi wa kuigiza kwa ufasaha
- kueleza maana ya msamiati uliotumiwa katika mchezo wa kuigiza
- kuonyesha ufahamu wa mchezo wa kuigiza kwa kujibu maswali
- kuigiza mchezo mfupi ili kukuza uwezo wa kujieleza
- kufurahia kusoma michezo na kuigiza
Mwanafunzi aelekezwe:
- kutafuta video ya mchezo wa kuigiza katika mtandao salama
- kutaja wahusika katika mchezo huo wa kuigiza
- kueleza maelekezo yaliyotumiwa katika mchezo huo wa kuigiza
- kuandika ujumbe wa mchezo huo wa kuigiza kwa ufupi
- kusomea wenzake ujumbe huo ili wautolee maoni
- kuendelea kufanya mazoezi ya kuigiza mchezo alichosoma kwa kutumia maelekezo yafaayo
1. Kwa nini maelekezo ni muhimu katika mchezo wa kuigiza? 2. Ni maelekezo gani yaliyotumiwa katika mchezo wa kuigiza uliotazama?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 125
Video ya mchezo wa kuigiza
Kifaa cha kidijitali cha kutazama video
Mtandao salama
Kutaja wahusika katika mchezo wa kuigiza Kueleza maelekezo katika mchezo wa kuigiza Kuandika ujumbe wa mchezo wa kuigiza Kuigiza mchezo kwa kuzingatia maelekezo
4 4
Sarufi
Mnyambuliko wa Vitenzi: Kauli ya Kutendana
Mnyambuliko wa Vitenzi: Kutendewa, Kutendeka na Kutendana
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- kutambua vitenzi katika hali ya kutendana katika matini ili kuvitofautisha
- kutumia vitenzi katika hali ya kutendana ipasavyo anapowasiliana
- kuchangamkia matumizi ya vitenzi katika hali ya kutendana katika mawasiliano ya kila siku
Mwanafunzi aelekezwe:
- kutazama picha zinazoonyesha vitendo (salimiana, agana)
- kujadili kinachotendeka kwenye picha hizo
- kusoma vitenzi kwenye picha hizo
- kueleza kuwa vitenzi hivyo viko katika kauli ya kutendana
- kutaja vitenzi vingine vitano katika kauli ya kutendana
- kuchora duara kwenye vitenzi katika kauli ya kutendana kwenye mraba
- kupigia mstari vitenzi vilivyo katika kauli ya kutendana kwenye sentensi
Kauli ya kutendana huonyesha nini?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 133
Picha zinazoonyesha vitendo katika kauli ya kutendana
Mraba wenye vitenzi mbalimbali
Sentensi zenye vitenzi katika kauli ya kutendana
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 136
Jedwali la kunyambua vitenzi katika kauli mbalimbali
Sentensi zenye nafasi za kujaza
Daftari la mwanafunzi
Kutambua vitenzi katika kauli ya kutendana Kutaja vitenzi katika kauli ya kutendana Kupigia mstari vitenzi katika kauli ya kutendana Kuchagua sentensi zenye vitenzi katika kauli ya kutendana
5 1
Kuandika
Kusikiliza na Kuzungumza
Insha za Masimulizi
Mazungumzo ya Kimuktadha: Miktadha Rasmi
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- kueleza sifa za insha ya masimulizi ili kuibainisha
- kuandika insha ya masimulizi kwa kufuata kanuni zifaazo
- kuchangamkia utunzi mzuri
Mwanafunzi aelekezwe:
- kuzingatia vidokezo alivyoandaa kuandika insha ya masimulizi kuhusu "Ziara ya Kuona Ndege wa Porini"
- kuandika insha isiyopungua maneno 150 kwa kuzingatia vigezo kama vile mada, utangulizi, mwili, na hitimisho
- kusoma insha aliyoandika kwa wenzake ili waisome na kuitolea maoni
- kurekebisha insha yake kulingana na maoni ya wenzake
- kuhifadhi nakala safi ya insha hiyo katika potifolio
Je, ni sifa zipi muhimu za insha ya masimulizi?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 127
Vidokezo vya insha ya masimulizi
Daftari la mwanafunzi
Potifolio
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 138
Picha za watu katika miktadha mbalimbali
Orodha ya miktadha rasmi na yasiyo rasmi
Chati ya miktadha rasmi
Kuandika insha ya masimulizi Kuzingatia muundo wa insha ya masimulizi Kusoma na kurekebisha insha ya masimulizi Kuhifadhi insha katika potifolio
5 2
MAGONJWA

Kusoma
Kusoma kwa Mapana: Matini
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- kutambua matini za aina mbalimbali za kusoma na kuchagua zinazomvutia
- kusoma matini alizochagua ili kufaidika na ujumbe na lugha iliyotumiwa
- kufurahia usomaji wa aina mbalimbali za matini ili kupanua mawazo yake
Mwanafunzi aelekezwe:
- kutembelea maktaba au mtandao salama
- kuchagua matini zinazomvutia
- kujaza jedwali la matini alizozichagua (k.v. majarida, vitabu, magazeti)
- kueleza sababu zinazomfanya avutiwe na matini hizo
- kusoma kimyakimya matini alizozichagua
- kueleza ujumbe unaojitokeza katika matini hizo
1. Ni habari zipi unazopenda kusoma kwenye matini? 2. Unachagua matini hizo kwa nini?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 141
Majarida, vitabu na magazeti
Jedwali la matini mbalimbali
Mtandao salama
Kuchagua matini zinazowavutia Kujaza jedwali la matini alizochagua Kueleza sababu za kuchagua matini fulani Kusoma matini aliyochagua
5 3
Kusoma
Sarufi
Kusoma kwa Mapana: Matini
Vinyume vya Vitenzi
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- kutambua matini za aina mbalimbali za kusoma na kuchagua zinazomvutia
- kusoma matini alizochagua ili kufaidika na ujumbe na lugha iliyotumiwa
- kufurahia usomaji wa aina mbalimbali za matini ili kupanua mawazo yake
Mwanafunzi aelekezwe:
- kusoma kimyakimya matini alizozichagua
- kueleza ujumbe unaojitokeza katika matini hizo
- kuandika ujumbe wa matini hizo kwa ufupi
- kuwasilisha muhtasari aliandika kwa wenzake
- kuomba wenzake wautoe muhtasari huo maoni
- kujadiliana na wenzake kuhusu ujumbe wa matini walizosoma
1. Je, ungehimiza mtu mwingine kusoma matini uliyosoma? Kwa nini? 2. Matini yako inakufunza nini kuhusu magonjwa?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 141
Matini alizochagua mwanafunzi
Daftari la mwanafunzi
Vifaa vya kidijitali
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 145
Picha zinazoonyesha vitendo kinyume
Jedwali la vitenzi na vinyume vyake
Chati ya maneno mbalimbali
Sentensi zenye vitenzi
Kusoma matini aliyochagua Kueleza ujumbe wa matini aliyosoma Kuandika muhtasari wa matini Kuwasilisha muhtasari kwa wenzake
5 4
Sarufi
Vinyume vya Vitenzi
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- kutambua vinyume vya vitenzi katika matini
- kuunda sentensi kwa kutumia vinyume vya vitenzi
- kuchangamkia matumizi ya vinyume vya vitenzi katika mawasiliano ya kila siku
Mwanafunzi aelekezwe:
- kutazama picha za shangazi anaanika nguo na shangazi anaanua nguo
- kusoma sentensi zilizo chini ya picha hizo
- kupigia mstari vitenzi katika sentensi alizosoma
- kueleza uhusiano uliopo kati ya vitenzi hivyo
- kuandika sentensi upya kwa kutumia vinyume vya vitenzi vilivyopigiwa mstari
- kutumia kinyume cha kitenzi kilicho mabanoni kujazia nafasi
- kutunga sentensi kutumia vinyume vya vitenzi
1. Ni vipi tunavyoundua vinyume vya vitenzi? 2. Matumizi ya vinyume vya vitenzi yana umuhimu gani katika mawasiliano?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 146
Picha za shangazi akianika na kuanua nguo
Sentensi zenye vitenzi vilivyopigiwa mstari
Sentensi zenye nafasi za kujaza
Orodha ya vitenzi
Kutambua vitenzi katika sentensi Kuandika sentensi kwa kutumia vinyume vya vitenzi Kujaza nafasi kwa kutumia vinyume vya vitenzi Kutunga sentensi zenye vinyume vya vitenzi
6 1
Kuandika
Kusikiliza na Kuzungumza
Insha za Maelezo
Mazungumzo ya Kimuktadha: Miktadha Rasmi
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- kutambua vifungu vya maelezo vilivyoandikwa kwenye matini mbalimbali
- kuandika insha ya maelezo kwa kufuata mtindo na muundo ufaao
- kuchangamkia utunzi mzuri wenye ujumbe mahususi
Mwanafunzi aelekezwe:
- kusoma insha ya maelezo kuhusu jinsi ya kudhibiti magonjwa
- kutaja mada ya insha hiyo
- kujadili ujumbe wa insha hiyo
- kutambua muundo wa insha hiyo (kichwa, utangulizi, mwili, hitimisho)
- kueleza sifa za insha ya maelezo
- kubainisha vipengele muhimu katika insha ya maelezo
1. Je, umewahi kuandika insha ya maelezo? 2. Uliandika insha ya maelezo kuhusu mada gani?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 142
Insha ya maelezo kuhusu jinsi ya kudhibiti magonjwa
Chati ya muundo wa insha ya maelezo
Orodha ya sifa za insha ya maelezo
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 139
Mazungumzo kati ya daktari na mgonjwa
Vifaa vya kidijitali kwa maigizo
Chati ya sifa za lugha rasmi
Kutambua vipengele vya insha ya maelezo Kubainisha utangulizi, mwili na hitimisho wa insha Kueleza ujumbe wa insha ya maelezo Kueleza sifa za insha ya maelezo
6 2
Kusoma
Sarufi
Kusoma kwa Mapana: Matini
Vinyume vya Vitenzi
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- kutambua matini za aina mbalimbali za kusoma na kuchagua zinazomvutia
- kusoma matini alizochagua ili kufaidika na ujumbe na lugha iliyotumiwa
- kufurahia usomaji wa aina mbalimbali za matini ili kupanua mawazo yake
Mwanafunzi aelekezwe:
- kutembelea mtandao salama na kutafuta matini kuhusu magonjwa
- kusoma matini anazochagua
- kueleza maana za maneno mapya anayopata kutoka kwenye matini
- kujadili ujumbe wa matini hizo na wenzake
- kuandika muhtasari wa matini alizosoma
- kushirikisha wenzake kuhusu mambo muhimu aliyojifunza kutoka kwa matini
1. Ni maneno gani mapya umejifunza kutoka kwa matini uliyosoma? 2. Unaweza kueleza ujumbe wa matini uliyosoma kwa njia gani?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 142
Mtandao salama
Matini mbalimbali za kidijitali
Kamusi ya Kiswahili
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 147
Jedwali la vitenzi na vinyume vyake
Sentensi zenye vitenzi
Orodha ya miktadha
Daftari la mwanafunzi
Kutafuta matini katika mtandao salama Kusoma matini aliyochagua Kueleza maana za maneno mapya Kuandika muhtasari wa matini
6 3
Kuandika
Kusikiliza na Kuzungumza
Insha za Maelezo
Tashbihi: Tashbihi za Tabia
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- kutambua vifungu vya maelezo vilivyoandikwa kwenye matini mbalimbali
- kuandika insha ya maelezo kwa kufuata mtindo na muundo ufaao
- kuchangamkia utunzi mzuri wenye ujumbe mahususi
Mwanafunzi aelekezwe:
- kujadili mada mbalimbali kuhusu magonjwa zinazoweza kuandikiwa insha ya maelezo
- kuchagua mada moja kati ya zile alizojadili
- kuandaa vidokezo vitakavyomwongoza kuandika insha hiyo
- kuandika insha isiyopungua maneno 150 kuhusu mada aliyoichagua
- kusomea wenzake insha aliyoandika ili waitolee maoni
- kurekebisha insha kulingana na maoni ya wenzake
1. Je, ni vipengele gani vya kuzingatia unapoandika insha ya maelezo? 2. Maua gani yanayosababisha magonjwa?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 143
Vidokezo vya kuandaa insha
Daftari la mwanafunzi
Kalamu na penseli
Mifano ya insha za maelezo
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 150
Picha za tashbihi za tabia
Vifaa vya kidijitali
Chati zenye tashbihi
Kuchagua mada ya insha ya maelezo Kuandaa vidokezo vya insha Kuandika insha ya maelezo Kusomea wenzake insha Kurekebisha insha
6 4
KUDHIBITI ITIKADI ZA KIDINI NA ZA KIJAMII

Kusoma
Sarufi
Sarufi
Matini ya Kidijitali
Nyakati na Hali: Hali ya Mazoea
Nyakati na Hali: Hali ya Mazoea
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- Kutambua na kuzingatia hatua za kiusalama katika matumizi ya vifaa vya kidijitali
- Kutambua na kufungua faili iliyo na kifungu cha kusoma ili kuimarisha umilisi wake wa kutumia tarakilishi
- Kusakura kwenye tovuti salama ili kupata vifungu vya kusoma
- Kuchangamkia matumizi ya vifaa vya kidijitali katika kutafuta na kusoma ujumbe
Mwanafunzi aelekezwe:
- Kutazama picha za vifaa vya kidijitali na kutaja majina yake
- Kujadiliana na wenzake kuhusu hatua za kiusalama wanazozingatia wanapotumia vifaa vya kidijitali
- Kuchagua hatua za kiusalama za kuzingatia wanapotumia vifaa vya kidijitali
- Kutaja mambo mengine ya kufanya ili kuwa salama mtandaoni
Ni hatua gani za kiusalama unazozingatia unapotafuta habari mtandaoni?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 154
Picha za vifaa vya kidijitali
Tarakilishi/vipakatalishi
Orodha ya hatua za kiusalama
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 159
Kapu maneno
Sentensi zenye vitenzi katika hali ya mazoea
Picha zinazoonyesha vitendo vya kila siku
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 161
Kapu la vitenzi
Sentensi zenye vitenzi katika hali ya mazoea
Kutambua hatua za kiusalama mtandaoni Kutaja majina ya vifaa vya kidijitali Kueleza umuhimu wa kutoa habari kwa wazazi/walezi/walimu
7 1
Kuandika
Kusikiliza na Kuzungumza
Kusoma
Insha ya Masimulizi
Tashbihi: Tashbihi za Tabia
Matini ya Kidijitali
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- Kutambua insha ya masimulizi kwa kuzingatia muundo
- Kuandika insha ya masimulizi kwa kufuata kanuni zifaazo
- Kuchangamkia utunzi mzuri wa insha
Mwanafunzi aelekezwe:
- Kusoma insha ya masimulizi "SHEREHE NILIYOHUDHURIA"
- Kutambua insha ya masimulizi, mada yake na muundo wake
- Kutambua utangulizi, mwili na hitimisho wa insha hiyo
- Kutambua maudhui ya insha hiyo
- Kujadiliana na wenzake kuhusu muundo na maudhui ya insha ya masimulizi
Ni mambo gani unayozingatia ili kuandika insha ya masimulizi ya kuvutia?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 156
Mfano wa insha ya masimulizi "SHEREHE NILIYOHUDHURIA"
Chati ya muundo wa insha ya masimulizi
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 151
Kifungu cha habari "Kijiji cha ltikadi"
Kapu la tashbihi
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 155
Tarakilishi/vipakatalishi
Mtandao
Faili zenye vifungu vya kusoma
Kutambua sehemu za insha ya masimulizi Kutambua mada ya insha Kutofautisha kati ya utangulizi, mwili na hitimisho
7 2
Sarufi
Nyakati na Hali: Hali Timilifu
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- Kutambua viambishi vya hali timilifu katika kitenzi
- Kutambua vitenzi katika hali timilifu katika matini
- Kutumia vitenzi vya hali timilifu katika sentensi
- Kufurahia matumizi ya hali timilifu katika mawasiliano
Mwanafunzi aelekezwe:
- Kutazama picha zinazoonyesha vitendo vilivyokamilika na kusoma sentensi zilizo chini ya picha hizo
- Kutambua vitendo katika sentensi vimetendeka muda upi
- Kutambua viambishi vya hali timilifu (me) katika sentensi
- Kupigia mstari viambishi vya hali timilifu katika vitenzi vilivyotolewa
- Kupigia mstari viambishi vya hali timilifu kwenye sentensi
Mambo gani ambayo umeyafanya muda mfupi uliopita?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 162
Picha zinazoonyesha vitendo vilivyokamilika
Kapu la vitenzi katika hali timilifu
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 163
Kadi za sentensi zenye vitenzi katika hali timilifu
Orodha ya vitenzi
Kutambua viambishi vya hali timilifu Kupigia mstari viambishi vya hali timilifu Kutunga sentensi zenye vitenzi katika hali timilifu
7 3
Kuandika
Kusikiliza na Kuzungumza
Kusoma
Insha ya Masimulizi
Kutoa Masimulizi
Kusoma kwa Ufasaha
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- Kuandika insha ya masimulizi kwa kufuata kanuni zifaazo
- Kuchangamkia utunzi mzuri wa insha
- Kufurahia kusimulia matukio kwa kufuata mpangilio mzuri
Mwanafunzi aelekezwe:
- Kuchagua mada kutoka orodha iliyotolewa kama "Ndoto ya Ajabu", "Itikadi za Kidini na za Kijamii", "Sherehe ya Kufana", n.k.
- Kuandika insha ya masimulizi isiyopungua maneno 150 kuzingatia muundo wa insha ya masimulizi
- Kuwasomea wenzake insha aliyoandika ili waitolee maoni
- Kuandika insha ya masimulizi kuhusu HARUSI NILIYOHUDHURIA kwenye tarakilishi
Unawezaje kupata kwa haraka hoja za kusimulia katika insha?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 158
Orodha ya mada za insha
Tarakilishi/vipakatalishi
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 167
Mifano ya masimulizi
Vifaa vya kidijitali
Picha
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 169
Picha ya mtu akisoma
Chati ya mambo ya kuzingatia katika kusoma kwa ufasaha
Kuandika insha ya masimulizi Kusomeana insha Kutolea maoni insha za wenzake
7 4
UWEKEZAJI

Sarufi
Sarufi
Sarufi
Ukanushaji: Nafsi na Wakati
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- Kutambua viambishi vya nafsi katika sentensi
- Kukanusha viambishi vya nafsi katika sentensi kwa usahihi
- Kutunga sentensi sahihi zenye viambishi vya nafsi na kuzikanusha
- Kufurahia ukanushaji wa viambishi vya nafsi katika sentensi
Mwanafunzi aelekezwe:
- Kutazama picha na kusoma sentensi zilizo chini ya picha hizo
- Kutambua viambishi vilivyoandikwa kwa rangi nyekundu
- Kutambua viambishi vya nafsi ya kwanza, ya pili na ya tatu
- Kutambua viambishi vya nafsi ya kwanza, ya pili na ya tatu katika umoja na wingi
- Kutambua viambishi vya nafsi kwenye sentensi zilizotolewa
Je, viambishi vya nafsi katika vitenzi ni vipi?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 174
Picha na sentensi
Chati ya viambishi vya nafsi
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 177
Michoro/picha
Tarakilishi/vipakatalishi
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 178
Kadi za sentensi zenye viambishi vya wakati
Chati ya viambishi vya wakati
Kutambua viambishi vya nafsi katika sentensi Kukanusha sentensi zenye viambishi vya nafsi Kutunga sentensi zenye viambishi vya nafsi
8 1
Sarufi
Kuandika
Kusikiliza na Kuzungumza
Ukubwa na udogo wa nomino
Baruapepe
Kutoa Masimulizi
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- Kutambua nomino zinazoanza kwa herufi m na zenye mzizi wa silabi mbili
- Kutambua nomino zinazoanza kwa herufi m katika hali ya ukubwa
- Kubadilisha nomino katika hali ya wastani kuwa katika hali ya ukubwa
- Kutumia nomino zinazoanza kwa herufi m katika hali ya ukubwa kwenye sentensi
Mwanafunzi aelekezwe:
- Kutazama picha na kutaja nomino zinazorejelewa katika picha hizo
- Kutambua herufi zinazoanza nomino hizo
- Kuhesabu silabi za nomino hizo baada ya kuondoa herufi m
- Kuchagua nomino zinazoanza kwa herufi m na zenye mzizi wa silabi mbili kwenye orodha iliyotolewa
- Kutazama picha zinazoonyesha tofauti kati ya hali ya wastani na hali ya ukubwa
Ni nomino gani unazoweza kutaja ukubwa wake?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 181
Picha za nomino
Chati ya nomino zinazoanza kwa herufi m
Kapu la maneno
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 172
Mfano wa baruapepe
Chati ya muundo wa baruapepe
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 168
Picha mbalimbali
Vifaa vya kidijitali
Kutambua nomino zinazoanza kwa herufi m na zenye mzizi wa silabi mbili Kubadilisha nomino kutoka hali ya wastani kuwa katika hali ya ukubwa
8 2
Kusoma
Sarufi
Kusoma kwa Ufasaha
Ukubwa na udogo wa nomino
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- Kusoma kifungu cha simulizi kwa kuzingatia matamshi bora, kasi inayofaa, sauti inayofaa na ishara zinazofaa
- Kutumia ishara zifaazo anapoisoma
- Kuchangamkia kusoma kwa ufasaha
Mwanafunzi aelekezwe:
- Kusoma kifungu "Bidii ya Marimari" kwa zamu akiwa katika kikundi
- Kusoma kifungu hicho kwa kuzingatia matamshi bora
- Kusoma kifungu hicho kwa sauti inayosikika vizuri
- Kusoma kifungu hicho kwa kasi inayofaa
- Kusoma kifungu hicho akiambatanisha ishara zinazofaa
- Kuhesabu maneno anayoweza kusoma kwa dakika moja
Je, unafanya nini ili kupata habari zilizoko katika kifungu simulizi kwa usahihi?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 170
Kifungu cha habari "Bidii ya Marimari"
Saa ya kupimia muda
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 184
Picha za nomino katika hali ya wastani na udogo
Chati ya nomino zinazoanza kwa herufi m katika hali ya udogo
Kusoma kwa kuzingatia matamshi bora Kusoma kwa kasi inayofaa Kusoma kwa sauti inayosikika vizuri Kutumia ishara zinazofaa wakati wa kusoma
8 3
Sarufi
Ukubwa na udogo wa nomino
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- Kutambua nomino zinazoanza kwa herufi n
- Kutambua nomino zinazoanza kwa herufi n katika hali ya ukubwa
- Kubadilisha nomino kutoka hali ya wastani kuwa katika hali ya ukubwa
- Kutumia nomino katika hali ya ukubwa kwenye sentensi
Mwanafunzi aelekezwe:
- Kutazama picha na kutaja nomino zinazorejelewa katika picha hizo
- Kutambua herufi zinazoanza nomino hizo
- Kuchagua nomino zinazoanza kwa herufi n kwenye ubao uliowekwa
- Kutazama picha zinazoonyesha tofauti kati ya hali ya wastani na hali ya ukubwa
- Kutambua njia za kuunda ukubwa wa nomino zinazoanza kwa herufi n
Ni nomino gani zinazoanza kwa herufi n?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 188
Picha za nomino zinazoanza kwa herufi n
Chati ya nomino katika hali ya wastani na ukubwa
Kutambua nomino zinazoanza kwa herufi n Kubadilisha nomino kutoka hali ya wastani kuwa katika hali ya ukubwa Kutunga sentensi zenye nomino katika hali ya ukubwa
8 4
Sarufi
Kuandika
Ukubwa na udogo wa nomino
Baruapepe
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:

- Kutambua nomino zinazoanza kwa herufi n
- Kutambua nomino zinazoanza kwa herufi n katika hali ya udogo
- Kubadilisha nomino kutoka hali ya wastani kuwa katika hali ya udogo
- Kutumia nomino katika hali ya udogo kwenye sentensi
Mwanafunzi aelekezwe:
- Kutaja nomino zinazoanza kwa herufi n
- Kutazama picha zinazoonyesha tofauti kati ya hali ya wastani na hali ya udogo
- Kutambua picha iliyo katika hali ya wastani na iliyo katika hali ya udogo
- Kueleza jinsi ya kubadili nomino nguruwe kutoka hali ya wastani kuwa katika hali ya udogo
- Kuchagua nomino zinazoanza kwa herufi n katika hali ya udogo kwenye baluni zilizotolewa
Ni nomino gani unazoweza kutaja udogo wake?
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 192
Picha za nomino katika hali ya wastani na udogo
Chati ya nomino zinazoanza kwa herufi n katika hali ya udogo
Kielekezi cha Kiswahili Gredi ya 5 uk. 173
Tarakilishi/vipakatalishi
Mtandao
Kutambua nomino zinazoanza kwa herufi n katika hali ya udogo Kubadilisha nomino kutoka hali ya wastani kuwa katika hali ya udogo Kutunga sentensi zenye nomino katika hali ya udogo

Your Name Comes Here


Download

Feedback