If this scheme pleases you, click here to download.
WK | KIPINDI | MADA KUU | MADA NDOGO | SHABAHA | SHUGHULI ZA UFUNZAJI | MASWALI DADISI | NYENZO | TATHMINI | MAONI |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
2 | 1 |
USALAMA NYUMBANI
Kusikiliza na Kuzungumza Kusikiliza na Kuzungumza |
Kusikiliza kwa Kufasiri
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
- -Kutambua ujumbe katika matini ya kusikiliza. -Kueleza uhusiano kati ya ujumbe wa matini na maisha ya kila siku. -Kujadili mafunzo yanayotokana na ujumbe wa matini. -Kujenga mazoea ya kuhusisha ujumbe katika matini na hali ya maisha ya kila siku. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kueleza masuala yanayozungumziwa katika matini aliyosikiliza kutoka kwa mwalimu, mgeni mwalikwa au katika vifaa vya kidijitali. -Kusikiliza matini katika vifaa vya kidijitali, kutoka kwa mwalimu au mgeni mwalikwa na kueleza uhusiano wa ujumbe wa matini hiyo na maisha ya kila siku. -Kujadili na wenzake mafunzo yanayotokana na ujumbe wa matini. -Kushirikiana na mzazi au mlezi kusikiliza na kuchanganua habari katika matini za aina mbalimbali kuhusu suala lengwa. |
Ni ujumbe gani uliowahi kuusikiliza katika matini ambao unafanana na matukio halisi katika jamii yako?
|
Oxford Fasaha Kiswahili pg 139
-Vifaa vya kidijitali -Mgeni mwalikwa -Mwongozo wa mwalimu -Kamusi |
Uchunguzi
-Maswali ya mdomo
-Maswali ya maandishi
-Kujitathimini
|
|
2 | 2 |
Kusoma
|
Kusoma kwa Kina: Tamthilia - Dhamira
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
- -Kueleza maana ya dhamira katika fasihi ili kuipambanua. -Kutambua dhamira katika tamthilia. -Kujadili dhamira katika tamthilia aliyosoma. -Kujenga mazoea ya usomaji wa kazi za kifasihi ili kujenga misingi ya uchambuzi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kusoma kielelezo cha tamthilia. -Kujadili kielelezo hicho cha tamthilia kinahusu nini. -Kubainisha lengo la mwandishi wa kielelezo hicho cha tamthilia. -Kueleza maana ya dhamira katika fasihi. -Kutambua dhamira katika kielelezo cha tamthilia. -Kujadili dhamira hizo. -Kuandaa maelezo mafupi kuhusu dhamira za tamthilia. -Kuwasilisha maelezo hayo darasani ili wenzake wayatolee maoni. |
Je, unafikiri mwandishi alikuwa na lengo gani katika tamthilia ambazo umewahi kuzisoma?
|
Oxford Fasaha Kiswahili pg 143
-Tamthilia -Vifaa vya kidijitali -Mwongozo wa mwalimu |
Uchunguzi
-Maswali ya mdomo
-Maswali ya maandishi
-Kujitathimini
|
|
2 | 3 |
Kusoma
Kuandika |
Kusoma kwa Kina: Tamthilia - Maudhui
Insha za Kubuni: Insha ya mdokezo |
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
- -Kueleza maana ya maudhui katika fasihi ili kuyapambanua. -Kutambua maudhui katika tamthilia. -Kujadili maudhui katika tamthilia aliyosoma. -Kujenga mazoea ya usomaji wa kazi za kifasihi ili kujenga misingi ya uchambuzi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kutazama picha zinazohusiana na usalama nyumbani. -Kujadili picha hizo zinahusu nini. -Kusoma tena kielelezo cha tamthilia kilichosomwa awali. -Kueleza masuala makuu yanayoangaziwa katika kielelezo hicho cha tamthilia. -Kueleza maana ya maudhui. -Kutambua maudhui katika tamthilia iliyosomwa. -Kujadili maudhui yanayojitokeza katika tamthilia. -Kuandika maelezo mafupi kuhusu maudhui hayo. -Kuwasilisha maelezo hayo darasani ili wenzake wayatolee maoni. |
Je, tamthilia uliyowahi kusoma ilikuwa inahusu nini?
|
Oxford Fasaha Kiswahili pg 146
-Tamthilia -Picha -Vifaa vya kidijitali -Mwongozo wa mwalimu Oxford Fasaha Kiswahili pg 150 -Kielelezo cha insha |
Uchunguzi
-Maswali ya mdomo
-Maswali ya maandishi
-Kujitathimini
|
|
2 | 4 |
Kuandika
Sarufi |
Insha za Kubuni: Insha ya mdokezo
Vivumishi vya Sifa |
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
- -Kueleza maana ya insha ya mdokezo ili kuipambanua. -Kubainisha aina za insha ya mdokezo. -Kujadili vipengele vya insha ya mdokezo. -Kuandika insha ya mdokezo kwa kuzingatia vipengele vya uandishi husika. -Kufurahia kuandika insha za mdokezo ili kukuza ubunifu. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kusoma insha ya mdokezo iliyoandikwa "Siku ya mvua". -Kutambua vipengele vya insha ya mdokezo vinavyojitokeza katika insha aliyosoma. -Kusakura mtandaoni na kusoma vielelezo vya insha za mdokezo. -Kujadili midokezo ya insha mbalimbali. -Kuandika insha ya mdokezo kwa kuzingatia anwani inayooana na kisa, kisa kinachooana na mdokezo, lugha inayofaa, na muundo wa insha. -Kuwasomea wenzake insha ya mdokezo aliyoandika ili waitolee maoni. -Kusahihisha insha yake kulingana na maoni ya wenzake. |
Insha ya mdokezo ni insha ya aina gani?
|
Oxford Fasaha Kiswahili pg 150
-Kielelezo cha insha -Vifaa vya kidijitali -Mwongozo wa mwalimu Oxford Fasaha Kiswahili pg 157 -Picha -Chati ya maneno |
Uchunguzi
-Maswali ya mdomo
-Maswali ya maandishi
-Kujitathimini
-Tathmini rika
|
|
3 | 1 |
Sarufi
|
Vivumishi Viashiria
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
- -Kutambua vivumishi viashiria katika matini. -Kutumia vivumishi viashiria ipasavyo katika matini. -Kuchangamkia matumizi ya vivumishi viashiria katika sentensi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kutazama picha mbalimbali na kujadili umbali wa vitu kutoka kwa mhusika. -Kutaja kauli ambazo wanafikiri kila mhusika anatamka. -Kueleza maana ya vivumishi viashiria. -Kucheza mchezo wa kutaja vivumishi viashiria vya karibu, mbali kidogo na mbali sana. -Kutambua vivumishi viashiria kutoka kwenye chati ya maneno. -Kupigia mstari vivumishi viashiria katika sentensi. -Kutunga sentensi akitumia vivumishi viashiria. -Kuandika aya fupi kuhusu usalama nyumbani akitumia vivumishi viashiria. |
Unafikiria vivumishi viashiria ni vivumishi vya aina gani?
|
Oxford Fasaha Kiswahili pg 161
-Picha -Chati ya maneno -Vifaa vya kidijitali -Mwongozo wa mwalimu |
Uchunguzi
-Maswali ya mdomo
-Maswali ya maandishi
-Kujitathimini
|
|
3 | 2 |
KUHUDUMIA WENYE MAHITAJI MAALUM
Kusikiliza na Kuzungumza Kusikiliza na Kuzungumza |
Usikilizaji Husishi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-kueleza maana ya usikilizaji husishi ili kuubainisha, -kujadili vipengele vya kuzingatia katika usikilizaji husishi, -kufanya mazungumzo yanayozingatia vipengele vya usikilizaji husishi, -kuchangamkia kushiriki katika usikilizaji husishi ili kujenga uhusiano mwema na wengine. |
- Kueleza maana ya usikilizaji husishi akishirikiana na wenzake.
-Kujadili vipengele vya kuzingatia katika usikilizaji husishi. -Kusikiliza mazungumzo kuhusu suala lengwa kutoka kwenye vifaa vya kidijitali akizingatia na kutambua vipengele vya usikilizaji husishi vilivyozingatiwa. -Kumsikiliza mwenzake, mwalimu au mgeni mwalikwa akisema kauli au akisoma vifungu vifupi kuhusu suala lengwa na kufasiri hisia zake. |
Unaposhiriki katika usikilizaji husishi, utazingatia nini ili kufanikisha usikilizaji?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 50
-Kifaa cha kidijitali -Kanda za sauti/video -Mgeni mwalikwa Oxford Fasaha Kiswahili uk. 51 |
- Kumakinikia jinsi mwanafunzi anavyotumia lugha katika mawasiliano
-Kujibu maswali
-Maigizo
-Mijadala
|
|
3 | 3 |
Kusoma
|
Ufupisho
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-kueleza maana ya ufupisho ili kuupambanua, -kujadili vipengele vya ufupisho wa kifungu, -kufupisha kifungu akizingatia vipengele vya ufupisho, -kujenga mazoea ya kuwasiliana kwa maelezo mafupi. |
- Kueleza maana ya ufupisho akishirikiana na wenzake.
-Kujadili vipengele vya ufupisho wa kifungu akiwa na wenzake. -Kusoma kifungu kuhusu suala lengwa katika matini andishi au ya kidijitali akishirikiana na wenzake. -Kutambua kwenye matini andishi au ya kidijitali habari za kimsingi katika makala na kuzieleza kwa usahihi kwa kuzingatia mtazamo wa matini katika matini ya kufupishwa. |
Unazingatia nini unapofupisha kifungu?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 52
-Vifaa vya kidijitali -Kifungu cha ufahamu |
- Kujibu maswali
-Kutoa muhtasari wa ufahamu
-Wanafunzi kufanyiana tathmini
|
|
3 | 4 |
Kusoma
Kuandika |
Ufupisho
Insha za Kubuni: Maelezo |
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-kueleza maana ya ufupisho ili kuupambanua, -kujadili vipengele vya ufupisho wa kifungu, -kufupisha kifungu akizingatia vipengele vya ufupisho, -kujenga mazoea ya kuwasiliana kwa maelezo mafupi. |
- Kueleza kwa maneno yake habari muhimu katika kifungu alichosoma.
-Kufupisha kifungu alichosoma kwa kuzingatia mpangilio ufaao wa habari sahihi kutokana na matini akishirikiana na wenzake. -Kuwawasilishia wenzake kazi yake ili waitolee maoni. -Kumweleza mzazi au mlezi namna ya kufupisha kifungu kwa kuzingatia mpangilio ufaao wa habari sahihi kutokana na matini. |
Unazingatia nini unapofupisha kifungu?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 53
-Vifaa vya kidijitali -Kifungu cha ufahamu Oxford Fasaha Kiswahili uk. 54 -Kielelezo cha insha ya maelezo |
- Potifolio
-Shajara
-Wanafunzi kufanyiana tathmini
|
|
4 | 1 |
Kuandika
Sarufi |
Insha za Kubuni: Maelezo
Vivumishi Vimilikishi na vya Idadi |
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-kutambua tamathali mbalimbali za lugha katika insha ya maelezo, -kueleza jinsi tamathali mbalimbali za lugha zinavyochangia kujenga picha dhahiri katika insha ya maelezo, -kuandika insha ya maelezo akitumia tamathali mbalimbali za lugha ili kujenga picha dhahiri, -kufurahia kuandika insha za maelezo akitumia tamathali mbalimbali za lugha ili kujenga picha dhahiri. |
- Kuandika insha ya maelezo akitumia tamathali mbalimbali za lugha ili kujenga picha dhahiri katika insha ya maelezo.
-Kuwasomea wenzake insha aliyoandika ili waitolee maoni. -Kushiriki na wenzake kutambua tamathali za lugha zilizotumika katika kila insha. |
Je, unatumia lugha ya aina gani wakati unapotaka kumweleza mtu kitu ili aweze kupata picha kamili?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 55-56
-Kielelezo cha insha ya maelezo -Vifaa vya kidijitali Oxford Fasaha Kiswahili uk. 57 -Chati -Kadi maneno -Kapu maneno |
- Kuandika tungo mbalimbali
-Potifolio
-Shajara
|
|
4 | 2 |
Sarufi
|
Vivumishi Vimilikishi na vya Idadi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-kutambua vivumishi vimilikishi na vya idadi katika matini, -kutumia vivumishi vimilikishi na vya idadi ipasavyo katika matini, -kuchangamkia matumizi ya vivumishi vimilikishi na vya idadi katika mawasiliano. |
- Kujaza nafasi katika sentensi au vifungu kwa kutumia vivumishi vimilikishi na vya idadi ipasavyo.
-Kutunga sentensi au vifungu vifupi kwa kutumia vivumishi vimilikishi na vya idadi akizingatia masuala mtambuko mbalimbali likiwemo suala la kuhudumia wenye mahitaji maalum. -Kumtajia mzazi au mlezi sentensi zenye vivumishi vimilikishi na vya idadi katika mazingira ya nyumbani. |
Je, kuna tofauti gani kati ya vivumishi vimilikishi na vya idadi?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 58-59
-Chati -Kadi maneno -Kapu maneno -Vifaa vya kidijitali |
- Kutunga sentensi
-Kazi mradi
-Kujaza mapengo
|
|
4 | 3 |
UHALIFU WA MTANDAONI
Kusikiliza na Kuzungumza Kusikiliza na Kuzungumza |
Uzungumzaji wa Papo kwa Hapo
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-kueleza maana ya uzungumzaji wa papo kwa hapo ili kuupambanua, -kutambua vipengele vya kuzingatia katika uzungumzaji wa papo kwa hapo, -kutoa uzungumzaji wa papo kwa hapo kwa kuzingatia vipengele vifaavyo vya uzungumzaji, -kuchangamkia kutoa uzungumzaji wa papo kwa hapo ili kufanikisha mawasiliano. |
- Kutambua maana ya uzungumzaji wa papo kwa hapo.
-Kutazama picha na kubainisha uzungumzaji wa papo kwa hapo. -Kujadili vipengele vinavyozingatiwa katika uzungumzaji wa papo kwa hapo. -Kusikiliza rekodi ya mazungumzo kwenye kifaa cha kidijitali na kutambua vipengele vya uzungumzaji wa papo kwa hapo vilivyotumika. |
Unazingatia mambo gani ili kufanikisha uzungumzaji wa papo kwa hapo?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 135-137
-Picha -Kifaa cha kidijitali -Rekodi ya uzungumzaji Oxford Fasaha Kiswahili uk. 137-138 -Vielelezo vya uzungumzaji wa papo kwa hapo |
- Kumakinikia jinsi mwanafunzi anavyotumia lugha katika mawasiliano
-Mijadala
-Maigizo
-Mazungumzo
|
|
4 | 4 |
Kusoma
|
Kusoma kwa Kina: Mandhari na Ploti katika Tamthilia
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-kutambua mandhari mbalimbali katika tamthilia, -kujadili umuhimu wa mandhari katika tamthilia, -kuchangamkia nafasi ya mandhari katika tamthilia. |
- Kueleza maana ya mandhari.
-Kutazama picha na kutambua mandhari zinazoonekana. -Kusoma kielelezo cha tamthilia na kubainisha mandhari yaliyotumika. -Kujadili umuhimu wa mandhari katika kielelezo cha tamthilia walichosoma. -Kutambua na kuandika kwa ufupi kuhusu mandhari ya kielelezo cha tamthilia. |
Ni mandhari gani unayokumbuka yaliyo katika tamthilia ulizowahi kusoma?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 139-144
-Picha za mandhari mbalimbali -Kielelezo cha tamthilia -Tamthilia iliyoteuliwa na mwalimu |
- Kujibu maswali
-Wanafunzi kufanyiana tathmini
-Mijadala
|
|
5 | 1 |
Kusoma
Kuandika |
Kusoma kwa Kina: Mandhari na Ploti katika Tamthilia
Viakifishi: Alama za Mtajo |
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-kutambua ploti ya tamthilia aliyosoma, -kujadili umuhimu wa ploti katika tamthilia, -kuchangamkia nafasi ya ploti katika tamthilia. |
- Kutazama picha na kueleza matukio yanayojitokeza.
-Kueleza maana ya ploti. -Kusoma tamthilia na kutambua ploti yake. -Kuandaa muhtasari kuhusu ploti ya tamthilia. -Kujadili umuhimu wa ploti katika tamthilia aliyosoma. -Kuwasilisha darasani uchambuzi wake kuhusu ploti ili wengine wautolee maoni. |
Ploti ina umuhimu gani katika tamthilia ulizowahi kusoma?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 144-147
-Picha mbalimbali -Tamthilia iliyoteuliwa na mwalimu Oxford Fasaha Kiswahili uk. 147-149 -Kadi maneno -Chati -Vifungu vya habari vyenye alama za mtajo |
- Mijadala
-Utafiti
-Kujibu maswali
-Potifolio
|
|
5 | 2 |
Kuandika
Sarufi |
Viakifishi: Mshazari
Ngeli na Upatanisho wa Kisarufi: Ngeli ya I-ZI |
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-kutambua matumizi ya alama ya mshazari katika matini, -kutumia alama ya mshazari ipasavyo katika matini, -kuonea fahari matumizi yafaayo ya alama ya mshazari katika matini. |
- Kusoma kifungu cha habari na kutambua alama za uakifishaji zilizotumika.
-Kutambua alama ya mshazari na kueleza jinsi ilivyotumiwa. -Kutaja matumizi tofauti ya alama ya mshazari. -Kutunga sentensi akitumia alama ya mshazari kwa kuzingatia matumizi tofauti. -Kusahihisha kifungu kilichotolewa kwa kuweka alama ya mshazari panapostahili. |
Je, alama ya mshazari hutumiwa vipi katika maandishi?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 150-153
-Kadi maneno -Chati -Vifungu vya habari vyenye alama ya mshazari Oxford Fasaha Kiswahili uk. 153-157 -Picha -Orodha ya nomino -Kifaa cha kidijitali |
- Kutoa muhtasari wa ufahamu
-Wanafunzi kufanyiana tathmini
-Kuandika kifungu kwa kuzingatia matumizi ya alama ya mshazari
|
|
5 | 3 |
Sarufi
|
Ngeli na Upatanisho wa Kisarufi: Ngeli ya I-I
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi vya ngeli ya I-I katika sentensi, -kutambua nomino za ngeli ya I-I katika matini, -kutumia nomino za ngeli I-I katika matini kwa kuzingatia upatanisho ufaao wa kisarufi, -kuchangamkia kutumia nomino katika ngeli ya I-I ipasavyo katika sentensi na vifungu ili kuimarisha mawasiliano. |
- Kutaja majina ya vitu vilivyo kwenye picha na majina hayo ni ya ngeli gani.
-Kujadili sababu za majina hayo kuwa katika ngeli husika. -Kusoma maelezo kuhusu ngeli ya I-I. -Kutambua nomino za ngeli ya I-I katika orodha ya nomino. -Kupigia mstari nomino za ngeli ya I-I katika sentensi mbalimbali. -Kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi vya ngeli ya I-I katika mafungu ya maneno. -Kutunga sentensi akitumia nomino za ngeli ya I-I. |
Je, ni majina yapi unayoyajua ya ngeli ya I-I?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 158-162
-Picha -Chati -Orodha ya nomino -Kifaa cha kidijitali |
- Kutambua k.m. kwenye orodha
-Kuambatanisha maneno lengwa
-Kujaza mapengo
-Kutunga sentensi
-Kazi mradi
|
|
5 | 4 |
MAJUKUMU YA MNUNUZI
Kusikiliza na Kuzungumza Kusikiliza na Kuzungumza |
Kusikiliza kwa Kina: Sauti /k/ na /gh/
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-kutambua sauti /k/ na /gh/ katika silabi na maneno, -kutamka sauti /k/ na /gh/ ipasavyo katika silabi na maneno, -kutumia maneno yenye sauti /k/ na /gh/ ipasavyo katika matini ili kuyatofautisha kimatamshi, -kuchangamkia matamshi bora ya sauti /k/ na /gh/ katika mazungumzo ya kawaida. |
- Kutambua sauti /k/ na /gh/ katika silabi na maneno.
-Kusikiliza mwalimu akitamka silabi zenye sauti /k/ na /gh/. -Kutamka silabi hizo na kutambua sauti /k/ na /gh/ zilizomo. -Kusikiliza rekodi ya kifungu kikisomwa kwenye kifaa cha kidijitali. -Kutambua maneno yenye sauti /k/ na /gh/ kutoka katika kifungu hicho. |
Ni maneno yapi unayoyajua yaliyo na sauti /k/ na /gh/?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 125-126
-Rekodi ya maneno yenye sauti /k/ na /gh/ -Kadi za maneno -Kifaa cha kidijitali Oxford Fasaha Kiswahili uk. 126-128 -Vitanzandimi -Jozi za maneno yenye sauti /k/ na /gh/ |
- Kumakinikia matamshi ya mwanafunzi
-Kujibu maswali
-Wanafunzi kufanyiana tathmini
|
|
6 | 1 |
Kusoma
|
Kusoma kwa Ufahamu: Kifungu cha Kushawishi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-kutambua habari mahususi katika kifungu cha ufahamu cha kushawishi, -kutabiri matukio katika kifungu cha ufahamu cha kushawishi, -kueleza maana ya msamiati na vifungu vya maneno katika kifungu cha ufahamu cha kushawishi, -kujadili ushawishi katika kifungu cha ufahamu cha kushawishi, -kuchangamkia usomaji wa ufahamu shawishi ili kukuza hamu ya ujifunzaji. |
- Kutazama picha na kujadili inachokionekana.
-Kutoa utabiri kuhusu kifungu watakachosoma kulingana na picha. -Kujadili jinsi ya kudondoa habari muhimu katika kifungu cha ufahamu. -Kusoma kifungu cha "Mwanatende". -Kudondoa habari mahususi kutoka kifunguni hicho. |
Je, ni kwa njia gani tunaweza kutambua ujumbe wenye lengo la kushawishi katika habari?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 128-131
-Picha -Kifungu cha ufahamu "Mwanatende" |
- Kujibu maswali
-Mijadala
-Kutoa muhtasari wa ufahamu
-Wanafunzi kufanyiana tathmini
|
|
6 | 2 |
Kusoma
Kuandika |
Kusoma kwa Ufahamu: Kifungu cha Kushawishi
Insha za Kubuni: Masimulizi |
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-kutambua habari mahususi katika kifungu cha ufahamu cha kushawishi, -kutabiri matukio katika kifungu cha ufahamu cha kushawishi, -kueleza maana ya msamiati na vifungu vya maneno katika kifungu cha ufahamu cha kushawishi, -kujadili ushawishi katika kifungu cha ufahamu cha kushawishi, -kuchangamkia usomaji wa ufahamu shawishi ili kukuza hamu ya ujifunzaji. |
- Kueleza maana ya msamiati uliopo katika kifungu cha "Mwanatende".
-Kueleza maana ya vifungu vya maneno. -Kujadili ni nani aliyeshawishiwa katika kifungu hicho. -Kueleza matokeo ya ushawishi uliofanywa. -Kusakura mtandaoni na kusoma kifungu chochote kinachoshawishi kununua bidhaa fulani. |
Je, ni kwa njia gani tunaweza kutambua ujumbe wenye lengo la kushawishi katika habari?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 131-133
-Kamusi -Kifaa cha kidijitali -Mtandao Oxford Fasaha Kiswahili uk. 133-135 -Insha ya masimulizi "Safari ya kesho hupangwa leo" |
- Kujibu maswali
-Mijadala
-Kutoa muhtasari wa ufahamu
-Wanafunzi kufanyiana tathmini
|
|
6 | 3 |
Kuandika
Sarufi |
Insha za Kubuni: Masimulizi
Ngeli na Upatanisho wa Kisarufi: Ngeli ya U-U |
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-kubaini wazo moja kuu la insha ya masimulizi atakayoandika, -kuandika insha ya masimulizi inayoendeleza wazo moja kuu katika kila aya, -kufurahia kuandika insha za masimulizi katika maisha ya kila siku akizingatia ujumbe uliotegemezwa kwenye wazo moja kuu. |
- Kutambua jinsi wazo "safari ya kesho hupangwa leo" lilivyokuzwa katika kila aya.
-Kuchagua mada ya kuandikia insha ya masimulizi. -Kujadili vidokezo vya mada hiyo na kuandika vidokezo. -Kuandika insha ya masimulizi isiyopungua maneno 300 akizingatia wazo moja kuu. -Kumsomea mwenzake insha aliyoandika ili aitoe maoni. |
Je, unawezaje kulikuza wazo vizuri katika insha ya masimulizi?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 135-138
-Vidokezo vya insha -Kifaa cha kidijitali Oxford Fasaha Kiswahili uk. 138-142 -Chati -Jedwali la nomino za ngeli ya U-U -Orodha ya nomino |
- Kuandika tungo mbalimbali
-Wanafunzi kufanyiana tathmini
-Potifolio
-Shajara
|
|
6 | 4 |
Sarufi
|
Ngeli na Upatanisho wa Kisarufi: Ngeli ya U-YA
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi vya ngeli ya U-YA katika sentensi, -kutambua nomino za ngeli ya U-YA katika matini, -kutumia nomino za ngeli U-YA katika matini kwa kuzingatia upatanisho ufaao wa kisarufi, -kuchangamkia kutumia nomino katika ngeli ya U-YA ipasavyo ili kuimarisha mawasiliano. |
- Kutaja majina ya vitu vilivyo na majina yaliyo katika ngeli ya U-YA.
-Kubaini kwamba nomino za umoja katika ngeli ya U-YA huanza kwa u- ilhali nomino za wingi huanza kwa ma-. -Kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi vya ngeli ya U-YA. -Kutambua nomino za ngeli ya U-YA kutoka kwenye orodha ya nomino. -Kutunga sentensi akitumia nomino za ngeli ya U-YA akizingatia upatanisho wa kisarufi. -Kuandika kifungu kuhusu majukumu ya mnunuzi akitumia upatanisho ufaao wa kisarufi wa ngeli ya U-YA. |
Je, ni vitu gani katika mazingira yako vyenye majina yaliyo katika ngeli ya U-YA?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 142-144
-Chati -Jedwali la nomino za ngeli ya U-YA -Orodha ya nomino -Kadi maneno |
- Kutambua k.m. kwenye orodha
-Kuambatanisha maneno lengwa
-Kujaza mapengo
-Kutunga sentensi
-Kazi mradi
|
|
7 | 1 |
KUKABILIANA NA HISIA
Kusikiliza na Kuzungumza Kusikiliza na Kuzungumza |
Hadithi: Hurafa na Hekaya
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
somo, -Kueleza maana ya hurafa na hekaya ili kuzibainisha. -Kusimulia hurafa na hekaya kwa kuzingatia vipengele vya uwasilishaji. -Kufurahia hurafa na hekaya kama vipera vya fasihi simulizi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kusikiliza kielelezo cha hadithi ya hurafa na hekaya kutoka kwa mwalimu, mgeni mwalikwa au kifaa cha kidijitali. -Kueleza maana ya hurafa na hekaya ili kuzibainisha akishirikiana na wenzake. -Kueleza ujumbe katika hurafa na hekaya. -Kujadili na mwenzake vipengele vya uwasilishaji wa hurafa na hekaya. |
Je, hadithi ambayo umewahi kusikiliza ilihusu wanyama gani?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 77
-Vifaa vya kidijitali -Kamusi -Maelezo ya somo -Mwongozo wa mwalimu -Mgeni mwalikwa Oxford Fasaha Kiswahili uk. 78 -Vielelezo vya hurafa -Vielelezo vya hekaya |
Uchunguzi
-Maswali ya mdomo
-Tathmini rika
-Maswali ya maandishi
|
|
7 | 2 |
Kusoma
|
Kusoma kwa Kina: Wahusika katika tamthilia
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
somo, -Kutambua wahusika katika tamthilia aliyosoma. -Kujadili sifa za wahusika katika tamthilia. -Kujenga mazoea ya usomaji wa kazi za kifasihi ili kukuza hamu ya ujifunzaji. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kutambua wahusika katika tamthilia aliyoisoma. -Kujadili na wenzake sifa za wahusika katika tamthilia iliyoteuliwa na mwalimu. -Kuigiza wahusika katika tamthilia akiwa na wenzake ili kukuza uelewa wa sifa zao. -Kueleza uhusiano kati ya wahusika katika tamthilia iliyoteuliwa na mwalimu. |
Ni mambo yapi yanayokuelekeza kuwaelewa wahusika katika tamthilia?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 80
-Vitabu vya tamthilia -Chati -Maelezo ya somo -Mwongozo wa mwalimu -Video |
Uchunguzi
-Maswali ya mdomo
-Mijadala
-Maswali ya maandishi
|
|
7 | 3 |
Kusoma
Kuandika |
Kusoma kwa Kina: Wahusika katika tamthilia
Barua ya Kuomba Msaada |
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
somo, -Kuchambua mafunzo yanayotokana na wahusika katika tamthilia. -Kutumia ujuzi wake kutathmini wahusika katika tamthilia. -Kujenga mazoea ya usomaji wa kazi za kifasihi ili kukuza hamu ya ujifunzaji. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kutazama video kuhusu wahusika katika tamthilia aliyosoma. -Kuandaa muhtasari kuhusu sifa za wahusika katika video aliyotazama. -Kujadili mafunzo yanayotokana na matendo ya wahusika akishirikiana na wenzake. |
Je, ni mambo gani tunayoweza kujifunza kutokana na wahusika wa tamthilia?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 81
-Vitabu vya tamthilia -Vifaa vya kidijitali -Maelezo ya somo -Mwongozo wa mwalimu -Video Oxford Fasaha Kiswahili uk. 82 -Nakala ya barua ya kuomba msaada -Chati -Vielelezo vya barua |
Uchunguzi
-Maswali ya mdomo
-Uwasilishaji
-Tathmini rika
|
|
7 | 4 |
Kuandika
Sarufi |
Barua ya Kuomba Msaada
Vinyume vya Vitenzi na Vielezi |
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
somo, -Kuandika barua rasmi ya kuomba msaada kwa kuzingatia ujumbe, muundo na lugha ifaayo. -Kutumia vipengele vya barua rasmi katika uandishi. -Kufurahia kujieleza ifaavyo kwa njia ya barua. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kuandika barua rasmi ya kuomba msaada kuhusu masuala mbalimbali na kuwasomea wenzake darasani ili waitolee maoni. -Kuandika barua ya kuomba msaada katika kifaa cha kidijitali na kuwasambazia wenzake kupitia mtandao ili waitolee maoni. |
Je, ni vipengele vipi unazingatia wakati unapoandika barua ya kuomba msaada?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 83
-Vifaa vya kidijitali -Karatasi -Maelezo ya somo -Mwongozo wa mwalimu -Vielelezo vya barua Oxford Fasaha Kiswahili uk. 84 -Kadi maneno -Kapu maneno -Mti maneno -Chati |
Tathmini rika
-Uchunguzi
-Kazi andishi
-Uwasilishaji
|
|
8 | 1 |
Sarufi
|
Vinyume vya Vitenzi na Vielezi
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
somo, -Kutambua vinyume vya vielezi katika matini. -Kutumia vinyume vya vielezi ipasavyo katika matini. -Kuchangamkia kutumia vinyume vya vielezi katika mawasiliano. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kujaza nafasi katika sentensi au vifungu kwa kutumia vinyume vya vitenzi na vielezi ipasavyo. -Kutunga sentensi au vifungu vifupi akitumia vinyume vya vitenzi na vielezi ipasavyo akizingatia masuala mtambuko mbalimbali likiwemo suala la kukabiliana na hisia. -Kusakura mtandaoni au kutafiti katika vitabu vya ziada ili kupata vinyume zaidi vya vitenzi na vielezi. |
Je, unajua vinyume gani vya vielezi?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 85
-Vifaa vya kidijitali -Chati -Maelezo ya somo -Mwongozo wa mwalimu -Kamusi |
Uchunguzi
-Maswali ya mdomo
-Zoezi la kuandika
-Tathmini rika
|
|
8 | 2 |
HAKI ZA WATOTO
Kusikiliza na Kuzungumza Kusikiliza na Kuzungumza |
Kuzungumza kwa Kutumia Vidokezo vya Hoja
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
somo, -Kutambua umuhimu wa kuzungumza kwa kutumia vidokezo vya hoja. -Kutambua miktadha katika jamii ambapo kuzungumza kwa kutumia vidokezo vya hoja hufanywa. -Kujenga mazoea ya kutumia vidokezo katika mazungumzo ili kufanikisha mawasiliano. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kueleza maana ya kuzungumza kwa kutumia vidokezo vya hoja. -Kujadili na wenzake umuhimu wa kuzungumza kwa kutumia vidokezo vya hoja. -Kutambua miktadha katika jamii yake ambamo anahitaji kuzungumza kwa kutumia vidokezo vya hoja. |
Kwa nini ni muhimu kuandaa vidokezo unapozungumza?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 86
-Chati -Maelezo ya somo -Mwongozo wa mwalimu -Vielelezo vya vidokezo -Vifaa vya kidijitali Oxford Fasaha Kiswahili uk. 87 -Vidokezo |
Uchunguzi
-Maswali ya mdomo
-Mijadala
-Tathmini rika
|
|
8 | 3 |
Kusoma
|
Kusoma kwa Mapana: Matini ya kujichagulia
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
somo, -Kuteua matini ifaayo ya kujisomea. -Kueleza ujumbe katika matini ya kujichagulia. -Kujenga mazoea ya kusoma matini mbalimbali katika maisha ya kila siku. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kuteua matini ifaayo ya kujisomea. -Kueleza ujumbe wa matini ya kujichagulia aliyoisoma. -Kutambua msamiati uliotumiwa katika matini ya kujichagulia (k.v. ya usalama barabarani (mfano; tabia hatarishi kwa watumiaji wengine wa barabara, kutoa maoni na kuripoti kuhusu tabia hatarishi) ya kisayansi, ya kisiasa, ya kihistoria, ya kifasihi,). |
Unavutiwa zaidi na nini unaposoma makala ya kujichagulia?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 88
-Vitabu mbalimbali -Majarida -Magazeti -Vifaa vya kidijitali -Maelezo ya somo -Mwongozo wa mwalimu |
Uchunguzi
-Maswali ya mdomo
-Mjadala
-Muhtasari
|
|
8 | 4 |
Kusoma
Kuandika |
Kusoma kwa Mapana: Matini ya kujichagulia
Insha za Kubuni: Insha ya maelezo |
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
somo, -Kutambua maana za msamiati na matumizi mengine ya lugha katika matini ya kujichagulia. -Kutumia ujuzi wake kuelezea maana ya msamiati. -Kujenga mazoea ya kusoma matini mbalimbali katika maisha ya kila siku. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kutumia kamusi kutafuta maana za maneno asiyoyajua. -Kujenga rekodi ya msamiati aliojifunza katika kitabu. -Kutunga sentensi akitumia msamiati katika matini aliyoisoma. -Kusakura mtandaoni na kujichagulia matini ya ziada kisha aisome. |
Unazingatia mambo gani wakati wa kusoma makala ya kujichagulia?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 89
-Kamusi -Vitabu mbalimbali -Vifaa vya kidijitali -Maelezo ya somo -Mwongozo wa mwalimu Oxford Fasaha Kiswahili uk. 91 -Vielelezo vya insha |
Uchunguzi
-Maswali ya mdomo
-Muhtasari
-Tathmini rika
|
|
9 |
LIKIZO FUPI |
||||||||
10 | 1 |
Kuandika
Sarufi |
Insha za Kubuni: Insha ya maelezo
Mnyambuliko wa Vitenzi: Kauli ya Kutendeka, Kutendewa na Kutendatenda |
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
somo, -Kuandika insha ya maelezo ipasavyo kwa kuzingatia vipengele vyake. -Kutumia aina mbalimbali za lugha katika uandishi wa insha. -Kufurahia kuandika insha za maelezo katika maisha ya kila siku. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kuandika insha ya maelezo kwa kuzingatia vipengele vifaavyo. -Kuwasomea wenzake insha aliyoandika au kuwasambazia kwenye vifaa vya kidijitali ili waitolee maoni. -Kushirikiana na wenzake kusahihisha insha walizoandika na kutoleana maoni kwa amani na upendo. |
Je, ni vipengele gani vya kuzingatia katika kuandika insha ya maelezo?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 92
-Vifaa vya kidijitali -Karatasi -Maelezo ya somo -Mwongozo wa mwalimu -Vielelezo vya insha Oxford Fasaha Kiswahili uk. 93 -Kapu maneno -Mti maneno -Kadi maneno -Chati |
Uchunguzi
-Tathmini rika
-Kazi andishi
-Uwasilishaji
|
|
10 | 2 |
Sarufi
|
Mnyambuliko wa Vitenzi: Kauli ya Kutendeka, Kutendewa na Kutendatenda
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
somo, -Kutambua kauli ya kutendatenda katika vitenzi. -Kutumia vitenzi katika kauli ya kutendatenda ipasavyo katika matini. -Kuchangamkia kutumia vitenzi katika kauli ya kutendatenda ipasavyo ili kuimarisha mawasiliano. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kugeuza vitenzi katika kauli ya kutendeka, kutendewa na kutendatenda. -Kujaza nafasi katika sentensi au vifungu kwa kutumia vitenzi katika kauli ya kutendeka, kutendewa na kutendatenda ipasavyo. -Kutunga sentensi au vifungu vifupi kuhusu suala lengwa kwa kutumia vitenzi katika kauli ya kutendeka, kutendewa na kutendatenda akizingatia masuala mtambuko mbalimbali likiwemo suala la haki za watoto. |
Kwa nini ni muhimu kujifunza kauli za vitenzi?
|
Oxford Fasaha Kiswahili uk. 94
-Chati -Kadi maneno -Mti maneno -Kapu maneno -Vifaa vya kidijitali -Maelezo ya somo -Mwongozo wa mwalimu |
Uchunguzi
-Zoezi la kuandika
-Tathmini rika
-Uwasilishaji
|
|
10 | 3 |
CITIZENSHIP
Kusikiliza na Kuzungumza Kusikiliza na Kuzungumza |
Kusikiliza kwa Makini
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-Kueleza habari katika matini ya kusikiliza. -Kukadiria maana ya msamiati mahususi na vifungu katika matini ya kusikiliza. -Kudondoa habari muhimu katika matini aliyosikiliza kwa kufuata mpangilio ufaao. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kusikiliza matini kutoka kifaa cha kidijitali au mwalimu wake. -Kutambua hoja muhimu katika habari aliyosikiliza kuhusu magonjwa yasiyoambukizwa. -Kueleza hoja muhimu aliyotambua kutoka matini aliyosikiliza. -Kukadiria maana ya msamiati mahususi na vifungu katika matini aliyosikiliza. |
Je, kwa nini ni muhimu kuwa na mpangilio ufaao wa hoja kutoka habari uliyosikiliza?
|
Oxford Fasaha Kiswahili, uk. 95
-Vifaa vya kidijitali -Kinasasauti -Projekta -Vidokezo vya kusikiliza Oxford Fasaha Kiswahili, uk. 96 -Chati zenye msamiati wa magonjwa yasiyoambukizwa |
Kujibu maswali
-Kufupisha matini
-Kudondoa hoja muhimu
-Kutoa maana ya maneno
|
|
10 | 4 |
Kusoma
|
Kusoma kwa Ufasaha
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-Kueleza vipengele vya kusoma kwa ufasaha ili kuvibainisha. -Kusoma kifungu kwa kuzingatia matamshi bora. -Kusoma kifungu kwa kasi ifaayo. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kujadiliana na wenzake vipengele vya kuzingatia katika kusoma makala kwa ufasaha. -Kutazama vielelezo vya video za watu wanaosoma kwa ufasaha makala. -Kusoma kifungu kuhusu magonjwa yasiyoambukizwa katika matini andishi au ya kidijitali akizingatia matamshi bora. -Kusoma kifungu kuhusu magonjwa yasiyoambukizwa kwa kuzingatia kasi ifaayo. |
Je, unaposoma kifungu unazingatia mambo gani ili kufanikisha usomaji?
|
Oxford Fasaha Kiswahili, uk. 97
-Vifaa vya kidijitali -Projekta -Video za mielelezo ya usomaji |
Kusoma kwa sauti
-Maigizo
-Wanafunzi kufanyiana tathmini
-Kusoma kifungu kwa kasi ifaayo
|
|
11 | 1 |
Kusoma
Kuandika |
Kusoma kwa Ufasaha
Insha za Kiuamilifu - Hotuba ya kutoa ufafanuzi |
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-Kusoma kifungu kwa kutumia sauti ipasavyo. -Kusoma kifungu kwa kuambatanisha ishara zifaazo. -Kuridhia kusoma makala kwa kuzingatia vipengele vinavyofanikisha mawasiliano. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kusoma kifungu akizingatia sauti ifaayo. -Kusoma kifungu kwa kuambatanisha ishara zifaazo panapofaa. -Kusoma mbele ya wenzake kazi yake ili wamtolee maoni. -Kushirikiana na mzazi au mlezi kusoma makala akizingatia vipengele vya usomaji bora. |
Je, unaposoma kifungu unazingatia mambo gani ili kufanikisha usomaji?
|
Oxford Fasaha Kiswahili, uk. 98
-Kifungu cha habari kuhusu magonjwa yasiyoambukizwa -Vifaa vya kidijitali Oxford Fasaha Kiswahili, uk. 99 -Vielelezo vya hotuba ya kutoa ufafanuzi -Vitabu mbalimbali |
Kusoma kwa sauti
-Maigizo
-Wanafunzi kufanyiana tathmini
-Kujibu maswali
|
|
11 | 2 |
Kuandika
Sarufi |
Insha za Kiuamilifu - Hotuba ya kutoa ufafanuzi
Aina za Sentensi - Sentensi changamano |
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-Kuandika hotuba ya kutoa ufafanuzi kwa kuzingatia vipengele vyake. -Kuchangamkia nafasi ya hotuba ya kutoa ufafanuzi katika mawasiliano. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kuandika hotuba ya kutoa ufafanuzi kuhusu magonjwa yasiyoambukizwa akizingatia ujumbe, lugha na muundo ufaao. -Kuwasomea wenzake hotuba aliyoandika ili waitolee maoni. -Kuandika hotuba ya kutoa ufafanuzi kuhusu suala linaloathiri jamii yao kisha amsomee mzazi au mlezi ili aitolee maoni. |
Ni mambo gani ya kuzingatia katika kutoa hotuba ya ufafanuzi?
|
Oxford Fasaha Kiswahili, uk. 100
-Mifano ya hotuba za kutoa ufafanuzi -Vifaa vya kidijitali -Chati zenye vidokezo vya muundo wa hotuba Oxford Fasaha Kiswahili, uk. 101 -Orodha ya sentensi -Kapu maneno -Chati yenye sentensi mbalimbali |
Kuandika hotuba ya kutoa ufafanuzi
-Wanafunzi kufanyiana tathmini
-Uwasilishaji wa hotuba
-Mjadala
|
|
11 | 3 |
Sarufi
|
Aina za Sentensi - Sentensi changamano
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-Kutambua sentensi changamano katika matini. -Kutumia sentensi changamano ipasavyo katika matini. -Kuonea fahari matumizi ya sentensi changamano katika mawasiliano ya kila siku. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kuwawasilishia wenzake darasani sentensi changamano alizotunga ili wazitathmini. -Kumtungia mzazi au mlezi sentensi changamano zinazohusu shughuli katika mazingira ya nyumbani. -Kutunga sentensi changamano kuhusu magonjwa yasiyoambukizwa na namna ya kujikinga. |
Ni nini tofauti kati ya sentensi changamano na aina zingine za sentensi unazozijua?
|
Oxford Fasaha Kiswahili, uk. 102
-Vitabu mbalimbali -Kadi maneno -Mifano ya sentensi changamano |
Kutunga sentensi
-Kurekebisha sentensi
-Wanafunzi kufanyiana tathmini
-Kuandika aya zenye sentensi changamano
|
|
11 | 4 |
Kusikiliza na Kuzungumza
|
Hadithi - Wahusika
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-Kutambua wahusika katika hadithi. -Kuchambua sifa za wahusika katika hadithi. -Kueleza mafunzo kutokana na wahusika katika hadithi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kutambua washiriki katika hadithi inayosimuliwa. -Kutambua wahusika katika hadithi inayosimuliwa. -Kutambua sifa za wahusika katika hadithi aliyosikiliza kutoka kwa mwalimu, mgeni mwalikwa au vifaa vya kidijitali. -Kuchambua wahusika katika hadithi aliyosikiliza. |
Je, hadithi uliyowahi kusimuliwa ilikuwa na wahusika gani?
|
Oxford Fasaha Kiswahili, uk. 103
-Hadithi zenye wahusika mbalimbali -Vifaa vya kidijitali -Picha za wahusika Oxford Fasaha Kiswahili, uk. 104 |
Kumakinikia jinsi mwanafunzi anavyotambua wahusika
-Kujibu maswali
-Mazungumzo
-Mijadala
|
|
12 | 1 |
Kusoma
|
Kusoma kwa Kina - Mbinu za Lugha
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-Kutambua mbinu za lugha katika tamthilia. -Kueleza umuhimu wa mbinu za lugha zilizotumiwa katika tamthilia. -Kufurahia kuchanganua matumizi ya mbinu za lugha katika fasihi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kutambua mbinu za lugha kwenye tamthilia. -Kueleza umuhimu wa mbinu za lugha zilizotumiwa katika tamthilia iliyoteuliwa na mwalimu. -Kuhakiki uwasilishaji wa wenzake kuhusu mbinu za lugha katika tamthilia na kuutolea maoni. |
1. Tamthilia hutumia mbinu gani za lugha?
-2. Mbinu za lugha zina umuhimu gani katika tamthilia?
|
Oxford Fasaha Kiswahili, uk. 105
-Tamthilia teule -Vitabu mbalimbali -Vifaa vya kidijitali |
Kutambua mbinu za lugha
-Kujibu maswali
-Kuchanganua mbinu za lugha
-Mijadala
|
|
12 | 2 |
Kusoma
Kuandika |
Kusoma kwa Kina - Mbinu za Lugha
Insha za Kubuni - Insha ya maelezo |
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-Kutambua mbinu za lugha katika tamthilia. -Kueleza umuhimu wa mbinu za lugha zilizotumiwa katika tamthilia. -Kufurahia kuchanganua matumizi ya mbinu za lugha katika fasihi. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kufanya utafiti maktabani au mtandaoni kuhusu matumizi ya mbinu za lugha katika tamthilia. -Kuwasilishia mzazi au mlezi uchambuzi wa matumizi ya mbinu za lugha katika tamthilia aliyosoma. -Kutambua na kuchambua mbinu za lugha katika tamthilia ya kuchaguliwa. |
1. Tamthilia hutumia mbinu gani za lugha?
-2. Mbinu za lugha zina umuhimu gani katika tamthilia?
|
Oxford Fasaha Kiswahili, uk. 106
-Tamthilia teule -Vitabu mbalimbali -Vifaa vya kidijitali Oxford Fasaha Kiswahili, uk. 107 -Vielelezo vya insha za maelezo -Kamusi |
Kutambua mbinu za lugha
-Kujibu maswali
-Kuchanganua mbinu za lugha
-Mijadala
|
|
12 | 3 |
Kuandika
Sarufi |
Insha za Kubuni - Insha ya maelezo
Ukanushaji kwa Kuzingatia Hali - Hali ya mazoea na Hali timilifu |
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-Kuandika insha ya maelezo inayodhihirisha sifa za mahali. -Kuonea fahari utoaji wa maelezo kamilifu kuhusu kitu au jambo. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kutumia lugha inayojenga picha ya kinachoelezewa. -Kuandika insha ya maelezo inayotoa sifa za mahali akizingatia muundo ufaao na inayohusisha kuheshimu tamaduni za wengine. -Kubuni insha ya maelezo inayotoa sifa za mahali kisha awasambazie wenzake mtandaoni ili waitolee maoni. -Kumsomea mzazi au mlezi insha ya kubuni aliyoandika ili aitolee maoni. |
Je, ni vigezo vipi vinavyotumika katika kuandika insha ya maelezo?
|
Oxford Fasaha Kiswahili, uk. 108
-Vielelezo vya insha za maelezo -Vifaa vya kidijitali -Kamusi Oxford Fasaha Kiswahili, uk. 109 -Chati zenye mifano ya sentensi -Kapu maneno |
Kuandika insha ya maelezo
-Mijadala
-Wanafunzi kufanyiana tathmini
-Kuwasilisha kazi
|
|
12 | 4 |
Sarufi
|
Ukanushaji kwa Kuzingatia Hali - Hali ya mazoea na Hali timilifu
|
Kufika mwisho wa funzo mwanafunzi aweze:
-Kutambua ukanushaji kwa kuzingatia hali ya mazoea na timilifu katika matini. -Kukanusha sentensi kwa kuzingatia hali ya mazoea na timilifu. -Kuchangamkia kukanusha sentensi katika hali ya mazoea na timilifu ili kukuza mawasiliano. |
Mwanafunzi aelekezwe:
-Kukanusha sentensi au vifungu alivyotunga kisha awatumie wenzake kupitia vifaa vya kidijitali au kuwasomea darasani ili wazitolee maoni. -Kukanusha sentensi katika hali ya mazoea na timilifu. -Kutunga sentensi zenye ukanushaji kuhusu kuheshimu tamaduni za wengine. |
1. Je, unapotaka kukanusha sentensi unazingatia nini?
-2. Je, ukanushaji wa hali ya mazoea na timilifu hutofautianaje?
|
Oxford Fasaha Kiswahili, uk. 110
-Chati zenye mifano ya sentensi -Kapu maneno -Vifaa vya kidijitali |
Kukanusha sentensi
-Kutunga sentensi
-Mijadala
-Wanafunzi kufanyiana tathmini
|
Your Name Comes Here